Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila 'RAY C' akimshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu aliompatia ikulu jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C (wa tatu kushoto), Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na Sarah Mtweve Dada yake Ray C


Na Freddy Maro, Ikulu

Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.

Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.

Kwa apande wake, Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray  C yamegharamiwa na Rais.