HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 30, 2013

LEMA AWASHUKIA, MKUU WA MKOA DODOMA, WAZIRI NCHIMBI


Na Bryceson Mathias, Dodoma

MBUNGE wa Arusha Mjini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amemchanachana kisiasa Mkuu wa Mkoa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi, Chama cha Mapinduzi (CCM) na Polisi akisema, Propaganda na Mbinu za kiitikadi za Kukiita Chama Chake ni Kikabila, Kidini, na Kiukanda zimefikia mwisho.

Lema alisema hayo Jana Jumanne, Januari 29, 2013 kwenye Uwanja wa Baruti karibu na Chako ni Chako ikiwa ni baada ya kuzuiwa kutumia Uwanja wa Central ambao ulikuwa umeombwa awali, ambapo wahusika kutishiwa wasiutoa uwanja huo kwa ajili ya Chadema kufanyia Mkutano hapo.

Akimuanika Dk. Nchimbi kisiasa, Lema aliwaambia wananchi uwajani hapo kwamba, Nasikia Mkuu wa Mkoa anayedai Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama mkoani hapa amezuia Mikutano ya Vyama vya Siasa mkoani Dodoma kwa sababu Bunge linaendelea na kuhoji,

“Mkuu wa Mkoa ni Nani kwenye Chama cha Siasa?  Huyu Mama mbona ana Kihelehele? Chama cha Siasa kilichosajiliwa hakiwezi kuzuiwa kufanya kazi na RC, maana kimesajiliwa ili kifanya kazi tangu Januari 1 hadi Desemba 31 ya Mwaka Mzima. Hawa ni Makada wa CCM mkiwaogopa watawanyanyasa.

“Nilipofungua Tawi letu Morogoro, Polisi walitusindikiza hadi tulipoondoka, lakini nilisikia Polisi na Viongozi wa Wilaya na Mkoa Dodoma wamezuia Mapokezi na Maandamano ya Mapikipiki kwa sababu ya Usalama! Usalama gani wakati Twiga na Pembe wanapakiwa wazima wazima!! wakiwepo?”

Alisema kuna wapuuzi waliunda Propaganda za kikabili wakiwahadaa wananchi wakidai, Chadema ni Chama cha Kikabila; “Kama ni cha kikabila basi CCM ni Shemeji zetu maana viongozi walio wengi wameoa Dada zetu wa kichaga na ipo siku moja tutawaambia wasiwapikie Chakula”, .huku akiwataja waliooa wachaga kwa majina akiwawauliza wananchi; Niongeze Mwingine?...nao wakiitikia ongeza!!.

Walipokwama Gia ya ukabila wakaanza ya Udini, Kama Chadema ni cha Kidini basi Pius Msekwa, Edward Lowasa, Fredrick Sumaye, Spika Anna Makinda, John Pombe Magufuli na wengine wakristo  watoke CCM waje Chadema maana ni Wakristo,, akidai Uongo huo ndio walioutumia kwa Chama cha Wananchi (CUF) na Seif Sharif Hamadi akalainika.

Lema hakuuma maneno na kumnyoshea Kidole Rais Jakaya Kikwete akionya akikubali kuendekeza Udini uendelee kama ambavyo Waziri wake Stephen Wassira aliongeza Mgogoro wa Kuchinja badala ya kusuruhisha Kanda ya Ziwa, itafika mahali kwa kuwa ndani ya Polisi, Jeshi, Usalama kuna Askari wa Dini mbalimbali, watagawanyika kidini na matokeo yake yatakuwa mabaya kwa upuuzi wa mtu mmoja.   

Aidha Lema aliwashangaa wanasiasa kuingilia mambo ya Ki-Imani  badala ya kuwajibika kwenye Nyanja zao ambazo zimewashinda kuzitendea kazi ili kuwakomboa wananchi wanaoteseka kwa kukosa msaada wa Elimu, Afya  na Maendeleo, Ingawa Tanzania ni ya Tatu kwa Dhahabu duniani na viongozi wake wapo.

Hata hivyo Lema aliwageukia Viongozi wa Chadema Dodoma akisema, hawakuwa na haja kuwa waoga wa vitisho na zuio la Polisi katika kumpokea Mbunge wao au kufanya mikutano. Alisema Bunge linakaa Dodoma kwa karibu mara Tatu, hivyo vyama haviwezi kufanya shughuli kwa miezi sita, wapi na wapi. “Hiyo hatutaikubali kama ni Noma na iwe Noma”.

Aidha Polisi waliovaa Kiraia huku wakiwa na Bunduki kwenye gari lao L/Rover 110, Lema aliwarejea akisema, “Hawa Polisi wajibu wao ni kutulinda na kutusimamia tukifanya mikutano ili kuwe na usalama, mkiona wanatumika vibaya ni kwa sababu wamepigika kama sisi, hapa tunawasaidia kuwakomboa ili ingalau nao familia zao ziie na kuishi vizuri, zinalala mahali pabaya, zinakula kisichoridhisha kama sisi”.

No comments:

Post a Comment

Pages