HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 28, 2013

REAL MADRID YAING’OA BARCELONA KOMBE LA MFALME


 Ronaldo akishangilia moja ya bao lake
 Sergio Ramos akiwa mgongioni kwa Ronaldo wakishangilia bao la uongozi
 Wachezaji wa Barca chini ya nahodha Carles Puyol wakilalamikia moja ya maamuzi ya refa
 Lionel Messi kulia na Cesc Fabregas kushoto wakiwa hawaamini kama ngoma imekula kwao Nou Camp
 Rafael Varane akiifungia Madrid bao la tatu kwa kichwa, akiwazidi kupaa mabeki wa FC Barcelona
 Hapa Gerard Pique akimwangusha chini Ronaldo na kusababisha Madrid kupewa penati
 Ronaldo kulia akifunga mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa chini na Pique
 Hapa Ronaldo 'aki-slide' kushangilia bao la pili aliloifungia Madrid
Kocha Jose Mourinho akimkumbatia Rafael Varane baada ya kuifungia Madrid

BARCELONA, Hispania

Beki Jordi Alba akaifungia bao la kufutia machozi Barca katika dakika ya 89, lakini halikutosha kuiepushia kichapo hicho, na kujikuta wenyeji hao wakikubali kufungwa nyumbani mabao matatu na Madrid kwa mara ya kwanza tangu Machi 2007

MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo usiku ya juzi alifunga mara mbili kuipa Real Madrid ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya FC Bracelona, katika mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Mfalme ‘King's Cup.’

Pambano hilo lilipigwa ndani ya dimba la Nou Camp jijini hapa, ambapo kwa ushindi huo sasa Madrid ilikuwa ikisubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Atletico Madrid na Sevilla, ili kujua mpinzani wake wa fainali ya michuano hiyo itakayopigwa Mei.

Ronaldo, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mechi sita mfululizo za mahasimu hao 'El Clasicos' akiwa ugenini, wakati alipotikisa nyavu kwa kwa mkwaju wa penati dakika ya 13 baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Gerard Pique.

Licha ya bao hilo, Barca iliendelea kumiliki mpira, huku Ronaldo akibaki kuwa mtu hatari pekee katika kikosi hicho, akifumua na kukosa mashuti kadhaa, kabla ya kufunga kwa mpira uliorudi ‘rebound’ ya Angel Di Maria dakika ya 57.

Ronaldo, ambaye amekuwa akilaumiwa kwa kushindwa kung’ara katika mechi muhimu, hilo likawa bao lake la 12 katika mechi 18 alizoicheza dhidi ya Barca tangu alipojiunga Madrid mwaka 2009 na ni mara yake ya pili kufunga mara mbili akiwa Nou Camp.

Madrid ikatia chumvi katika donda la mechi ya awali wakati Raphael Varane, ambaye aliisawazishia Madrid katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 kwenye dimba la Santiago Bernabeu, – alipounganisha kona nyavuni dakika ya 68 kuipa Madrid bao la tatu.

Beki Jordi Alba akaifungia bao la kufutia machozi Barca katika dakika ya 89, lakini halikutosha kuiepushia kichapo hicho, na kujikuta wenyeji hao wakikubali kufungwa nyumbani mabao matatu na Madrid kwa mara ya kwanza tangu sare ya 3-3 Machi 2007.

SuperSport.com

No comments:

Post a Comment

Pages