HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 20, 2013

JWTZ LATOA UFAFANUZI KUHUSU AJIRA

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo  : “N G O M E”                Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo  :                              DSM  22150463  
                                                                     Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                            DAR ES SALAAM,19                                                                Septemba, 2013.
Tele Fax                                         : 2153426
Barua pepe          : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                       : www.tpdf.mil.tz

Taarifa kwa vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa taarifa zilizoenea kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi (sms) na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba JWTZ limeanza kuajiri wataalamu Jeshini (Professionals) siyo kweli na halina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia mitandao ya kijamii au kupitia simu za mikononi.

          Kwa kawaida, utaratibu wa kujiunga na Jeshi hutangazwa kwenye Vyombo vya Habari pale ambapo Jeshi linahitaji kuandikisha askari wapya.  JWTZ huelekeza utaratibu wa kuzingatia katika kuwasilisha maombi husika kwa taarifa hii, wananchi wote wanatahadharishwa kuhusu ujumbe huo unaoelekea kusababisha usumbufu kwa wananchi na JWTZ.  Taarifa hiyo haijatolewa na JWTZ hivyo wananchi wajihadhari na yeyote atakayejitokeza kuwarubuni na hatimaye kutapeliwa kwa namna yoyote.
                       
Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi

Dar es salaam, Tanzania

20 comments:

  1. Wale wote wanaotangaza habari hizi potofu, nashauri watafutwe kisha wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia kama hizi.

    ReplyDelete
  2. nia umriwa miaka ishirini elimu kidato cha nne division 4 alama 28 ninaniaya dhati ya kujiunga ili kulinda taifa langu.sijajua nifanyeje

    ReplyDelete
  3. nia umriwa miaka ishirini elimu kidato cha nne division 4 alama 28 ninaniaya dhati ya kujiunga ili kulinda taifa langu.sijajua nifanyeje

    ReplyDelete
  4. jina naitwa chris nimeitimu kidato cha sita na nilienda jeshi kama mijibu wa sheria hko kigoma hvyo nlipenda sana kuendelea najeshi na nazisubir kwa hamu hizo nafasi kwan nimejifunza mengi sana jeshini na nataman nije nisaidie watu wanaoitaji msaada kupitia jeshi mimi kama ntapata nafasi hyo ya kuajiliwa naomba sana na napenda sana nilinde wanachi na mali zao.

    ReplyDelete
  5. vp kuhusu umri wa kujiunga ukiwa na profesional

    ReplyDelete
  6. umri mwisho miaka 33 kwa professional

    ReplyDelete
  7. samahani ningependa kujua utaratibu wa kutuma maombi ya kujiunga na JWTZ

    ReplyDelete
  8. lakini rushwa inatunyima haki sisi tusio na uwezo na tuna vigezo vyote

    ReplyDelete
  9. nipo kasulu nimemalizaforn four divition 32 nina certificate ya ICT (information technology) ntapata jeshi coz nalipenda sana jeshi

    ReplyDelete
  10. hiyo miaka 33 kwa professionals ni kwa level gani ya elimu kati ya cheti,stashahada na shahada?

    ReplyDelete
  11. watu waongo kama hao ni kunyonga tu na si kukaa kucheka nao kisa uliwahi soma nae.

    ReplyDelete
  12. wote mnaopenda kujiunga na jeshi fateni utaratibu uliopo na sio vinginevyo,

    ReplyDelete
  13. Kuna gharama gani nikitaka kujiunga na jeshi?

    ReplyDelete
  14. naitwa thadei andrew mkaz wa dsm nmemariza kidato cha nne2012 n anmejiunga na chuo cha ufundi miaka 2 level2 fani ya fitter mechanics pia na AUTO ELECTRICAL morogoro je naweza pata nafasi ya kujiunga n jesh????? miaka yngu 22 plz nalipendaa jeshi nanipotayar kuli2mikia 0718029761 namb zngu km ntapata nafasi iyo

    ReplyDelete
  15. naitaji kujiunga na jeshi,eleimu yangu Diploma in accountancy and finance na pia ni mwanafunzi wa Open University mwaka wa kwanza Bachelor degree of Business management in Accounting. Msaada tafadhali mwenye uelewa au anayeweza kuniunganisha na wahusika. napenda sana jeshi. namba zangu ni 0757206540

    ReplyDelete
  16. Mwaka huu tunapataje kujiunga na jeshi la wana nchi haswa kwa wale ambao tume enda kwa mujibu Wa sheria operation magufuli

    ReplyDelete
  17. Kwa mwaka huu itakuwaje napenda kulitumikia taifa langu ajira za jwtz

    ReplyDelete
  18. sa kwa wale wamemalza fom 6na hawajapangiwa jkt na wanampango wa kujiunga na jeshi wanafanyaje

    ReplyDelete

Pages