HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 02, 2014

DIAMOND ATAMANI KUZAA NA WEMA SEPETU

Na Elizabeth John
STAA wa muziki nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’,  amesema kuwa anatamani kuwa na mtoto ili aweze kwenda sawa na wasanii wengine na angependa mpenzi wake Wema Sepetu ndiye awe mama wa mtoto huyo.

Alisema  anatamani kupata mtoto kutokana na kuwa wasanii wengi kwa sasa wana watoto na hivyo mara nyingi wanapenda kuzunguka nao maeneo mbalimbali.

“Ni jambo la faraja kuwa na mtoto kwani mara nyingi ndio anakuwa mtu wako wa karibu na hivyo ninatamani kwa kiasi kikubwa kuwa na mtoto,” alisema.

Msanii huyo alisema kuwa pia anawaomba mashabiki wake waendelee kumpa ushirikiano kwani bila wao yeye asingekuwepo sehemu alipo kwa sasa na pia anashuru kwa sapoti ambayo anaipata.

Diamond ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo kutokana na ubora wa mashairi ya kazi zake ambayo yanakubalika katika jamii inayomzunguka.
Hivi sasa mkali huyo anatamba na ngoma yake ya ‘My Number one Remex’ ambayo ameshirikiana vema na mkali kutoka Nigeria, Davido.

1 comment:

  1. that is what we call maturity Diamond i will also love to see you and wema bringing life into the world

    ReplyDelete

Pages