HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 23, 2014

Wadau wahimizwa kupiga kura KTMA
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandhi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu mchakato wa upigaji kura za wasanii wa Kilimajaro Music Award.

Na Clezencia Tryphone

WAKATI Tuzo za wasanii za Kilimanjaro Music Award zikitarajiwa kutimua vumbi Mei 3 mwaka huu, wadau wa muziki nchini wametakiwa kuitumia vema wiki ya mwisho ya upigaji kura katika kinyang’anyiro hicho cha (KTMA 2014).

Lengo kubwa la kuwataka wadau kupiga kura hasa wiki hii ni kuwawezesha wasanii, bendi na wateule wengine kushinda ili waweze kufanikiwa kupata tuzo katika ‘Usiku wa Tuzo’ utakaotimua vumbi katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo, kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), George Kavishe, mchakato umeenda vizuri tangu Aprili Mosi ulipoanza hadi sasa, ambako majaji watatumia wiki hii kutoa asilimia zao 30.

“Kuna asilimia 70 ya kura za wadau zinaendelea kupokelewa, lakini pia majaji nao wataitumia wiki hii kufanikisha asilimia 30 ya maamuzi yao kwa wateule. Tunawasisitiza mashabiki wahakikishe wanatumia fursa iliyosalia ili kufanikisha ushindi kwa wasanii/vikundi wavipendavyo,” alisema Kavishe.

Aliongeza kuwa, mchakato huo uko chini ya majaji waliobobea 15 wanaoufahamu vema muziki, ambao baadhi yao ni waalimu na wanamuziki mahiri, hivyo haki itatendeka na washindi wa kweli watapatikana.

Alisema, anaimani kubwa na majaji hao kwani hakuna mtu anayemfahamu jaji mpaka sasa, na kama kuna mtu anahitaji kuwatambua majaji anaweza kuwaona na kutoa sababu maalumu ya kutaka kuwafahamu majaji hao na wao kumpatia orodha nzima.

Huku Mwakilishi wa Kampuni ya Auditax, Straton Makundi, alibainisha kuwa, lengo la kuwepo kwa majaji hao katika mchakato huo ni kusimamia haki katika mchakato, kutoa miongozo ya upigaji kura, kutunza kumbukumbu na kuhesabu kura zote.

No comments:

Post a Comment

Pages