HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 20, 2014

Zaidi ya 60 watimkia Chadema, Mtendaji kata atoa Vitisho

Na Bryceson Mathias, Santilya Mbeya

WANACHAMA zaidi ya 60 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Jojo, Kata  ya Santilya, Mbeya vijijini, kwa mwezi mmoja sasa wametimka na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kiasi cha kumtia hofu Mtendaji wa Kijijiji hicho na kutoa vitisho.

Mtendaji huyo, Anderson Yamaliha, alijikuta akitishika na timka tika hiyo, iliyompelekea kutoa vitisho kwa waliohama kwamba warejee kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) haraka iwezekanavyo na wasipofanya hivyo watabambikiziwa kesi na kuchukuliwa hatua kali.

Mtendaji Yamaliha alipotafutwa kwenye simu 07689503390 ajibu tuhuma zake, Simu ya Mlinzi  huyo wa Amani hakujibu, na alipoandikiwa Ujumbe Mfupi hakujibu ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Jojo, Nelson Mwasile, alitoa ufafanuzi kuwa amepata malalamiko ya vitisho atayashughulikia.

“kuna taarifa kwamba ya kwamba vijana wa Chadema wamekataa kufanya Shughuli za Maendeleo na kazi za kijiji, kulikopelekea wao kukamatwa na Mtendaji na kudaiwa kuwa wamepigwa na Askari Mgambo na kudaiwa wametishiwa kubambikiziwa kesi, nitawakutanisha na kumaliza mgogoro huo”.alisema Mwasila.

Vijana waliohamia Chadema na kujiunga na ‘Red Brigade’ ambao wamechangia kuwafanya wanakijiji wengi wahame na kujiunge na Chadema, wameapa hawawezi kurejea, na kuwataka wazazi wao wanaosumbuliwa na mtendaji huyo kuwa warejee CMM, wampuuze.

Katibu wa Chadema Jojo, Osia Mwapepu amethibitisha kuwepo Mgogoro wa kutoelewana na Vijana wake wa Chadema, na kumekuwa na vitisho vinavyotolewa na Mtendaji wanaojiunga na Chama chake, ambapo alithibitisha wanachama 60 hadi 100 CCM wamehamia Chadema, ila nao wamepoteza wanachama wanne na Kiongozi mmoja.

No comments:

Post a Comment

Pages