HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 30, 2014

MAMIA WAMLAKI DIAMOND PLATINUMZ DAR


NA ELIZABETH JOHN
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ amewataka Watanzania kuendelea kumpa sapoti katika kazi zake kwa lengo la kuendelea kuiwakilisha vema tasnia ya muziki katika mataifa mbalimbali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana baada ya kuwasili nchini akitokea Marekani katika utoaji tuzo za AFRIMMA zilizofanyika usiku wa kuamkia Julai 28.

Diamond alishinda tuzo mbili za msanii bora wa kiume Afrika Mashariki na wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘My Number One’ alioimba na mkali kutoka Nigeria, Davido.

Katika mapokezi hayo, Diamond alipokelewa na mamia ya Watanzania ambapo kila mmoja aliyefika katika uwanja huo alitamani kumpa mkono wa hongera msanii huyo.

“Naomba sapoti mnayonionesha sasa hivi muendelee nayo, nashukuru mungu kwa kuniwezesha kufika hapa najua ni kutokana na sapoti zenu hivyo nawashukuru sana,” alisema Diamond.

Mtanzania mwingine aliyeshinda katika tuzo hizo ni mwadada Judith Wambura ‘Lady JayDee’ ameshinda msanii bora wa kike wa Afrika Mashariki na mtayarishaji bora wa muziki huo Afrika Mashariki ni Sheddy Clever.

No comments:

Post a Comment

Pages