HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 30, 2014

Mayanga avipa somo vilabu vya ligi kuu


Na Kenneth Ngelesi, MBEYA
 
KOCHA msadizi wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Salum Mayanga (pichani), amezitaka timu zinazoshiriki Ligi Kuu  Tanzania Bara kutumia mji wa Tukuyu kama sehemu ya mazoezi ya maandalizi kutoka na eneo hilo kuwa tulivu kwa ajili ya wachezaji.

Wito huo alitoa juzi Mjini Tukuyu wakati wa mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania ambayo imepiga kambi mjini hapa kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa marudiano  dhidi ya timu ya Taifa ya Msumbiji the Mambas unao tazamiwa kufanyika wiki ijayo.

Akizungumza na Tanzania daima  Kocha  huyo alisema kuwa mazingira ya mji wa Tukuyu ni mazuri  kwa kupiga kambi iwe kwa timu ya taifa ama vilabu vya ligi kuu kwani hakuna bugza kama ilivyo kwa Da-es-salaam.

Aliongeza  ni vema kwa timu za ligi mkuu kutimia maeneo kama yale kwani yanautulivu wa hali juu hivyo kumfanya mchezaji kuwa makini wakati wote.

‘Unajua hawa wachezaji wetu wakiwa jiji Dar-es-salaam wanakuwa na mambo mengi  ikingatiwa wengine ni wajaeriamalio  hivyo kia mara wanaomba ruhusa kwenga kuangalia miradi yao lakini kwa jhuyku ni ngumu hata linapo tokea tatizo anaishi kupiga simu, bali angfkuwa Dar angelazimika kuomba ruhusa’alisema Mayanga.

Hata hivyo kocha huiyo alisema kuwa anashangazwa na watu waloiko kuwa wanabeza uamuzi wa TFF kuatua mji huo kwa jili ya kambi ya Stars kwani mazimngira yeki mazuri kuliko watu wanavyo dhani kutokana na ulivu uliiopo.

Mbali na hali ya utulivu lakini pia hali ya hewa katika mji wa Tukuyu nzuri hivyo ameviasa  vilabu kutumia mazingira kama hayo kwa ajili ya  maandalizi kwa ajili ya michezo ya ligi kuu hata vilabu vinavyo jiandaa na michezo ya kimataifa.

Akizungumzia hali ya kambi hiyo Kocha huyo msadizi alisema kuwa ipo vizuri na ari ya wachezaji ipo juu na kwamba jana timu hiyo ilitazamiwa kurejea jiji Dar es Salaam tayari kwa safari ya kuelekea mjini Maputo kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

No comments:

Post a Comment

Pages