HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 24, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAANDALIA FUTARI WANANCHI WA PEMBA

Baadhi ya waumini wa Nini ya Kiislamu pamoja na wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba wakifutari pamoja hapo Ikulu ya Wete futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akawakilishwa kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ,h. Mohamed Aboud Mohamed (katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi kulia yake na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa wakijumuika na wananachi wa mikoa miwili ya Pemba kwenye futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitoa shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Kikwete mara baada ya futari ya pamoja kwa wananchi wa mikoa miwili ya Pemba.
  Balozi Seif akiwaaga na baadhi ya wananchi wa mikoa miwili ya pemba waliohudhuria futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete hapo Ikulu ya Wete Pemba.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na mmoja wa watoto walioshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Dk. Mrisho Kikwete hapo wete Pemba.

            xxxxxxxxxxxxxxxxx
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini kuendelea
kushikamana kwa lengo la kutekeleza maamrisho ya dini yao
kama inavyoagiza wakati wote.

Balozi Seif alitoa himizo hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri
  ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya futari ya Pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete kwa ajili
ya Wananchi wa Miko miwili ya Pemba hapo katika Majengo ya
Ikulu ya Serikali ya Muungano yaliyopo  Mjini Wete
Pemba.

Balozi Seif alisema njia ya kusimamisha mshikamano kwa
waislam hupatikana katika mjumuisho wa makundi ya ibada
akiyataja kuwa ni pamoja na madrsasa, sala pamoja na
mikusanyiko ya kufutari kwa pamoja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema
kitendo cha Rais Kikwete cha kukutanisha waumini na baadhi
ya wananchi katika maeneo tofauti Nchini kwa ajili ya futari
  ya pamoja ni moja ya njia ya kuwajengea waumini hao
ushirikiano utakaoongeza mapenzi baina yao.

Balozi Seif aliwatakia funga njema pamoja na kusherehekea
kwa amani na upendo siku kuu ya Idd el fitri waumini wote wa
  Zanzibar.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa mikoa miwili ya
Pemba Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi
alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.
Jkaya Mrisho Kikwete kwa moyo wake wa kutekeleza ibada
  hiyo.

Mh. Dadi alisema mpango huo wa Rais Kikwete ambao pia
hufanywa ba baadhi ya Viongozi wa wengine wa juu hapa
  nchini, wakiwemo pia wale wa Taasisi za umma na binafsi
  hutoa faraja kwa waumini ambao hali yao ya kipato ni duni
  katika kujipatia futari.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Pages