HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 22, 2014

Rungwe waasawa kuanzisha miradi ya ufugaji wa nyuki


Na Keneth Ngelesi, Rungwe 

WANANCHI waishio katika vijijini vilivyopo kando kando ya  lango kuu la kuingilia Mlima Rungwe  wameashwa kuwatumia watalaamu waliopo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kubuni na kuibua miradi ya kuichumi ambayo ni rafiki wa mazingira.


Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Festo Sikagonamo Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linajuhusha na uhifadhi wa Mazingira Elimisha wakati wa kutoa elimu ya ufungaji wa nyuki kwa njia ya kisasa kwa wananchi ya kijiji cha Syukula Wilayani hapa.


Akizungumza na wananchi hao Sikagonamo aliwataka  kuwa wabunifu hasa katika uibuaji wa miradi ambayo ya kujikwamua kiuchumi wakati huo huo ikawa ni njia moja wapo ya kuifadhi  mazingira ambayo kwa hivi sasa yameanza kuharibiwa.


Alisema kuwa taasisi hiyo imeamua kujikita zaidi kutoa elimu ya ufugaji wa nyuki kutokana miradi hiyo kuitaji mtaji mdogo na kwamba mwanachi wa kawaida  anaweza kumudu huku akiwa anashirika kampeni za uifadhi wa mazingira.


Alisema kuwa endapo wananchi hao wataitikia mwito huo wanaweza kuondokana na umasikini kwani soko la bidhaa zinazo tokana na nyuki ikiwemo asali ni  kubwa ndani ndani na nje ya nchi.


Aliongeza kuwa mbali la soko la ndani lakini pia bidha hizo ambazo ni pamoja asali inaweza kuuzwaasa kwa watalii ambao wamekuwa wakifika  katika mlima huo na vivutio vingene vilivyopo katika Wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla.


Alisema kuwa Wilaya ya Rungwe imejaliwa uoto wa asili mzuri na rafiki  kwa ufugaji wa nyuki na kwamba wakazi  katika Wilaya hiyo hawajazitumia vyema fursa zilizopo, ambapo zingetumika vyema umasikini kwa wananchi wa Wilaya hiyo ingekuwa ni hadidhi.


Kwa upande wake Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Busokela Wilaya ya Rungwe  Anamary Joseph ambaye ni miongoni mwa watalaamu walio fundisha mada mbalimbali za ufugaji wa nyuki na uhifadhi wa mazingira aliwataka wananchi wa kijiji hicho walio shiriki mafunzo hayo kuwa mabalozi kwa wale walioshindwa kushiriki mafunzo hayo.


Aidha alisema kuwa ni vema wananchi hao wakaanzisha miradi hiyo kupitia vikundi na kwamba taasisi ya Elimisha kushirikiana na Serikali watakuwa tayari kutoa mitaji kwa pamoja na kutoa vifaa kwa ajili ya miradi hiyo.


Afisa huyo alibainisha vifaa ambavyo vimesha nunuliwa na vinasubiriwa kugawia kwa vikundi ambavyo vitakuwa vipo trayari kuanzisha mradi wa ufugaji wa nyuki ni Masanduku,kwa ajili ya Mizingi, na vifaa vingine pam oja na kuwa taftia soka na bidhaa zitokanazo na ufugaji nyuki.


Akitoa shukurani kwa niaba ya wananchi walioshiriki Mafunzo hayo Mwenyekiti wa kamati ya Mazingira kijiji hapo Dickson Mwamakula alishukuru hatua ilichulkulia na Tasisi hiyo ya mazingira na kwamba elimu hiyo imefika mwafaka na imepokelewa kwa Mikono miwili.


Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakichukulia nyuki kama adui lakini kwa elimu iliyo tolewa na wataalamu wanaamini kabisa itasaidi kuondoka na umasikini kwani mchanganuo uliotolewa unaonyesha wazi nyuki mazao yatokanayo na nyuki yakitumika vyema yanaweza kuwa sadia wananchi kupiga teke umasikini.

No comments:

Post a Comment

Pages