HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 30, 2014

WATU 17 WAFA KATIKA AJALI YA BASI DODOMA

 Basi la Moro Best linavyoonekana baada ya kupata ajali.
Wakati sherehe za sikukuu ya Idd -El Firt zinaelekea ukingoni Taifa limepatwa na msiba mkubwa baada ya watu 17 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Moro Best kupata ajali mbaya eneo la Pandambili katikati ya Dodoma na Morogoro .

Akizungumza na mtandao wa matukio daima.co.tz kutoka eneo la tukio mmoja kati ya mashuhuda wa ajali hiyo Joseph Mtweve  alisema kuwa tukio limetokea eneo hilo la Pandambili wakati lori lililokuwa limebeba mabomba kutoka Morogoro kwenda Dodoma kujaribu kulipita gari jingine mbele eneo ambalo lina kona na hivyo kugongana na basi hilo uso kwa uso.

Alisema kuwa basi hilo lilikuwa likitokea Dodoma kuelekea mkoani Morogoro na kuwa katika ajali hiyo watu zaidi ya 12 walikufa papo hapo na wengine watano wanasadikika kufia njiani wakati wakikimbizwa Hospitali kwa matibabu zaidi.

Miongoni mwa  waliopoteza maisha katika ajali  hiyo inadaiwa pamoja na  dereva wa  basi hilo japo  jitihada za kupata  undani  wa  tukio  hilo  kupitia kwa  jeshi la polisi  zinaendelea kufanyika na mtandao huo.

No comments:

Post a Comment

Pages