Na Bryceson Mathias, Dodoma
MSAIDIZI wa Askofu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Samwel
Mshana, ameijia juu Serikali akisema Mchakato wa kupata Katiba Mpya usiwe wa
Chama Kimoja, hivyo wanawake wasilala usingizi wakahukumiwa, maana Yesu anakuja.
Akifungua Tamasha la siku
tatu la Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la
Makao Makuu Agosti 28 mwaka, Mshana alinukuu maandiko ya Mathayo 25:1-12 kuhus Wanawali
10, ambapo Watano walikuwa na Busara, Watano Wapumbavu.
“Yesu alisema, ‘Mimi ni
Njia Kweli na Uzima’, hivyo Mwanamke mwenye mafuta anayetegemea Kweli, hawezi kugombana na Ndoa yake, Viongozi
wa Kanisa na Serikali, na hawezi kutaka Katiba ya Chama au Kundi fulani,
atataka inayounganisha Vyama na Dini zote.
Wanawake msitumiwe
vibaya na Vyama vya Siasa, Makundi yoyote au Mtu binafsi, maana kwa kufanya
hivyo mtakuwa mnapoteza heshima na Busara yenu iliyo katika Zaburi 68:11 ‘Bwana
analitoa Neno lake, Wanawake watangazao habari ni Jeshi kubwa”.alisema Mshana’.
Wanawake watangazao
habari ni Jeshi kubwa ni Kauli Mbiu ya Tamasha hilo la Wanawaka wa KKKT Jimbo
la Makao Makuu Dodoma, ambayo itaambatana na Mafundisho ya Maadili ya Mwanamke
katika Kanisa, Ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia kwa wakati huu.
Askofu Mshana amelaani
Mauaji ya Wanawake na Albino yaliyoshamiri katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa,
Arusha na pengineyo, ambapo amesema Kanisa litaendelea kumuomba Mungu likipinga
Watu waovu wanaotaka kutatua mambo yao kwa kutenda vitendo Viovu.
Hata hivyo Mshana ameitaka
Serikali kutumia Mamlaka yake kuhakikisha inakomesha mauaji hayo badala ya kuwa
na Maneno mengi ya kuwatumainisha Wananchi kwenye Majukwaa ya Kisiasa lakini hawachukui
hatua zinazowahakikishia watu Usalama wa Maisha na Mali zao.
No comments:
Post a Comment