HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 28, 2014

Castle lite yatoa zawadi kwa washindi sita

Meneja Msaidizi wa Bia ya Castle Lite, Victoria Kimaro akizungumza wakati wa kutangaza washindi sita wa kwanza wa shindano la Castle Lite Yacht Party jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Bia hiyo, Geofrey Makau. (Picha na Francis Dande) 

DAR ES SALAAM, Tanzania

Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) leo imetangaza washindi wa wiki ya kwanza ya promosheni yake mpya inakayojulikana kama “Lite Up The Weekend”. Promotion hii ya aina yake hapa nchini iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwezi Agosti, na itakayodumu  kwa kipindi cha miezi mitatu hadi mwezi Octoba 2014.

Akizungumza katika uzinduzi huo, meneja wa Bia ya Castle Lite Geoffrey Makau alisema; Bia ya Castle Lite kama ilivyowatangazia Watanzania  hapo awali juu ya promosheni hii kubwa na ya aina yake nchini na leo wameanza kuwapata washindi wao wa kwanza ambao wameweza kujishindia kitita cha shilingi laki moja kwa kila mmoja (100,000). Jumla wamepatikana washindi 6 katika wiki hii ya kwanza. 

Hii ni promosheni kubwa inayoendeshwa nchi nzima. Na washindi wetu wa leo walishiriki kwenye hii promosheni kupitia chupa za bia ambapo waliweza kutuma nambari ya siri iliyopo chini ya kizibo cha bia ya Castle Lite.
 Tunawajulisha wateja wetu wapendwa wa castle lite kuwa tumewaandalia zawadi mbalimbali zitakazokuwa zikitolewa kila wiki, ikiwa ni pamoja na zawadi za pesa taslimu kama ambavyo tunawaona washindi wetu wa leo wakijishindia kitita cha fedha taslimu.

Pamoja na pesa taslimu vili vile kuna zawadi nyingine kem kem za kushindaniwa kama; zawadi za vifaa vya kusikilizia muziki (headfone), tshirts, kofia  pamoja na tiketi za kuhudhuria matamasha mbalimbali yaliyodhaminiwa na Castle lite lakini zawadi kubwa zaidi ni ile ya washindi kupata fursa ya kusherehekea kwenye VIP Party ndani ya Boti la kifahari. Sherehe hii itajulikana kama “Castle Lite VIP Yacht Party”

Napenda kuwakumbusha wateja kuwa namna ya kushiriki katika shindano hili ni kununua bia ya Castle Lite ya chupa yenye ujazo wa mililita 375 au 330 na kuangalia chini ya kizibo cha Bia, ambapo utakuta namba za siri, kisha utatuma namba hizo kwenda 15499 au kutembelea tovuti yetu ambayo ni, www.castlelite.co.tz, ili upate nafasi ya kushinda zawadi za kila wiki au zawadi kubwa ya “Castle Lite VIP Yacht Party”.

Kwa upande wake muwakilishikutoka Castle lite Victoria Kimaro alisema kwa kipindi hiki cha promosheni, bia  hiyo pia imeelezea jinsi ya kushiriki kwenye promosheni hii kupitia ujumbe maalumu uliopo kwenye lebo ya nyuma ya chupa ya Castle Liteili kuweza kumpatia mteja na mshiriki wa shindano hili urahisi wa kutambua namna ya kupata maelekezo ya kushiriki.

Victoria alisema mabadiliko haya ya nembo hiyo ni kwaajili ya kipindi cha miezi mitatu tu ambapo yatafikia ukomo pale shindano litakapo malizika rasmi. Promosheni hii pia itapewa msukumo mkubwa kupitia Radio, ambapo wapenzi wa Castle Lite watapigiwa simu na watatakiwa wapokee kwa kuanza na neno ya “Lite Up My Weekend”. wateja watakaofanya vizuri watapata zawadi mbalimbali kila wiki. Alisema Makau.

No comments:

Post a Comment

Pages