Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi kwa furaha wakati akielekea
ukingoni mwa Mto Kilombero kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu
juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Anaoongozana nao ni pamoja na Waziri wa
Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina
Kombani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (kushoto) na Mama
Salma Kikwete (nyuma ya Rais) PICHA
NA IKULU.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Pamoja
naye ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais),
Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga
Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mbunge wa Mama Salma Kikwete
(nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa
Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara (TANROADS) Bw. Patrick Mfugale juu ya ujenzi wa daraja la kudumu juu
ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John
Pombe, Magufuri akifuatiwa na Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani Kilombero mkoa
wa Morogoro Agosti 20, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi
la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani Kilombero
mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014
k1
na k2: Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa
kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa
wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan
hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.
mo28:Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu madawati mapya ya shule ya msingi ya
Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500
na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini
aina ya Graphite na Nickel mkoani wa Morogoro Agosti 20, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete na mmoja wa
wanafunzi wa shule ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo
kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd
inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani
Morogoro Agosti 20, 2014.
No comments:
Post a Comment