Watuhumiwa wa kesi ya Ugaidi wakiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo.
Wakiingia Mahakamani.
Sheikh Farid akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam huku akiambatana na watuhumiwa wenzake.
WASHITAKIWA 20 wanaokabiliwa
na mashtaka mbalimbali ya kigaidi hapa nchini leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, huku wakilalamikia kupata mateso wakiwa mahabusu.
Washtakiwa hao wameyasema hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salama, mbele ya Hakimu Mkazi
Hellen Liwa, baada ya waendesha mashitaka wa Serikali, Pita Njike na George Balasa kuiomba mahakama iwaruhusu kuwachukua
washitakiwa saba ili waende kuhojiwa kwa upelelezi zaidi.
Washitakiwa walioombwa kwenda
kuhojiwa ni Sheikh Farid Hadi Ahmed, Ramadhani Alawi, Amour Juma, Mohamed
Yusuph, Nassoro Abdalah, Hamis Amour na Hassani Bakari.
Ndipo mshitakiwa namba moja
katika kesi hiyo Sheikh Farid Hadi Ahmed ambaye pia ni kiongozi wa Jumuiya ya
Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) alisema kuwa mara ya kwanza
walipoombwa mahakamani hapo ili kwenda kuhojiwa, hawkufanyiwa ustarabu wala
ubinadamu. "tulihojiwa tukiwa uchi" amesema Sheikh Farid.
“Watu wameumizwa vibaya
hayasemeki, kuna mtu hapa anakojoa damu wiki ya pili sasa lakini hatujapewa
matibabu yoyote,kwahiyo muheshimiwa hakimu tunaomba mtutafutie Dactari aje
afanye uchunguzi juu ya afya zetu.Vinginevyo muheshimiwa siku utaletewa maiti
hapa mahakamani” alisema Farid.
Naye mshitakiwa namba 12
katika kesi hiyo Salum Ali Salum,alidai mbele ya mahakama hiyo kuwa ameingiliwa
kinyume na maumbile kinguvu, na
ameimgiziwa chupa na mti sehemu zake za nyuma.
“Nakuomba muheshimiwa Hakimu
kama unaweza twende faragha nikakuonyeshe,hapa nilipo sehemu zangu za nyuma
zinavuja ,nimeingizwa jiti mpaka limekatikia,kwahiyo muheshimiwa naomba
nipatiwe matibabu”alisema Salum.
Hakimu aliwataka washitakiwa
walete malalamiko yao kwa njia ya maandishi,washitakiwa wite walirudishwa
rumande hadi Septemba 3 mwaka huu.
Wakati huohuo mahakama hiyo
imelazimika kuiahilisha kesi inayowakabili viongozi wawili wa Jumuiya ya Uamsho
na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) ), Mselem Ally Mselem na Abdallah
Said Alli (Madawa),kwasababu mshitakiwa Mselem Ally Mselem hakuweza kufika
mahakamani hapo kwakuwa ni mgojwa.
Akiahiahilisha kesi hiyo
Hakimu Mkazi Agustino Mbando,Waendesha mashitaka wa serikali Peter Njige na
George Balasa,walidai mshitakiwa namba moja hakufika mahakamani ,kwahiyo
wakamuomba hakimu apange tarehe nyingine ya kuja kutajwa tena kwa kesi hiyo.
Awali washitakiwa hao
walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwamo la
kuingiza watu kufanya vitendo vya kigaidi nchini.
Hakimu Mbando aliihailisha
kesi hiyo mpaka Septemba 3 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment