HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 10, 2014

KIFARU CHA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) CHAGONGA NYUMBA NA KUUWA WATU WATATU MKOANI MTWARA



Kifaru kilichokuwa kikisafiri kutoka Mtwara kwenda Lindi kikiwa kimeacha njia na kugonga nyumba usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mnolela Lindi vijijini, kusababisha vifo vya watu watatu katika ajali hiyo. (Na Mpiga Picha Wetu)

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ), kwa masikitiko makubwa linatoa taarifa kuhusu ajali iliyotokea alfajiri ya tarehe10 Septemba 2014 mnamo saa 11:20 katika kijiji cha Mnolela (Lindi vijijini), 

wakati Wanajeshi wetu walipokuwa katika msafara wa kawaida kwa kutumia magari maalumu ya kubeba askari kutoka Mtwara kwenda Masasi.

Katika msafara huo gari moja lilipata ajali kwa kugonga nyumba na kusababisha kifo cha mama mmoja (Raia) pamoja na wanajeshi wawili.   Aidha, majeruhi wanne Wanajeshi walikimbizwa katika Hospitali ya Ligula iliyopo Mtwara kwa matibabu. 

Jeshikwahivisasalimeungananafamiliazamarehemukatikauombolezaji.

Uchunguziwa kina kuhusuchanzo cha ajali unafanyika kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

 Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
MakaoMakuuyaJeshi, Upanga S.L.P  9203,   Dar es Salaam, Tanzania.
 
Kwa Mawasiliano zaidi: 0754 - 270136

No comments:

Post a Comment

Pages