HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 21, 2014

KINANA ATINGA KIHABA MJINI LEO, AKAGUA NA KUFUNGUA MIRADI YA MAENDELEO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuvyeka miti wakati wa uzinduzi wa kambi ya Umoja wa Vijana wa CCM, ya mafunzo ya kilimo katika eneo la Boko Timiza, Kibaha mjini mkoa wa Pwani. Katika kambi hiyo vijana wanatarajiwa kufanya mafunzo ya kilimo kwenye shamba la ekari 25. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye kiwanja unakofanyika ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani, baada ya kuzindua ujenzi huo leo, Septemba 19, 2014.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Kushoto ni Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka.
 Kinana akipata burudani ya Ngonjera kutoka kwa vijana Chipukizi baada ya kuzindua ujenzi Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mjini leo. Wapili kulia ni Nape.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimfurahia Chipukizi wa CCM,  Suma Iddi, aliyekuwepo wakati akizindua ujenzi Ofisi ya CCM, wilaya ya Kibaha mjini
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua tangi la maji alipokagua ujenzi wa mradi wa maji katika kitongoji cha  Muheza, wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kuhusu wodi ya wagonjwa mahututi iliyopo kwa sasa kwenye hospitali hiyo, ambapo alisema bado inahitajika kuwepo dawa za kutosha kuliko ilivyo sasa.
Mganga Mkuu wa  Huduma za Afya Hospitali ya Tumbi Dk. Peter Dattani akieleza changamoto mbali mbali walizonazo hospitali ya Tumbi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alieleza bado hospitali hiyo inahitaji vifaa na madawa kwani inapokea majeruhi kwa asilimia mia moja.

No comments:

Post a Comment

Pages