HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 18, 2014

MWENYEKITI WA CHADEMA AHOJIWA POLISI KWA SAA TANO

Baadhi ya wapenzi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakishangilia baada ya gari lililokuwa limembeba Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alipowasili leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, kwa mahojiano yaliyodumu kwa saa tano kuanzia saa 11:10 asubuhi hadi 3:17 alasiri. (Picha zote na Joseph Senga)
Mawakili wawili kati ya watano, Mabere Marando (kushoto) na Profesa Abdallah Safari, wakiwasili katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, ambako Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alihojiwa na Polisi.
 Mwenyekiti wa Chama cha DP, Christopher Mtikila akihojiwa na askari Polisi, alipowasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa bajaji, ambako Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alihojiwa na Polisi.
Mmoja wa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye jina lake halikuweza kupatikana, akipewa kibano na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), nje ya Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam.
 Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakimpa kichapo mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Josephat Isango, nje ya Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam.
Askari wa Kikosi cha Mbwa, wakiranda na mbwa wao nje ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, kuwatawanya wananchi na waandishi wa habari.
Mbowe akitoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi baada ya kupata dhamana.

No comments:

Post a Comment

Pages