HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 20, 2014

Mtwara wapewa Mafunzo ya Maafa

 Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa imetoa Mafunzo ya Dhana ya Maafa kwa wataalamu kutoka Halmashauri na Manispaa ya Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuandaa Mpango wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa. Miongoni mwa masuala yanaoelezwa ni pamoja na jinsi ya Kujiandaa na Maafa, Kukabili, Kuzuia na namna ya kurudisha hali baada ya Maafa kutokea. Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
20 Septemba,2014
Mada zikitolewa kuhusu mafunzo ya kukabiliana na maafa mkoani Mtwara, mafunzo hayo yametolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa wataalam wa Halmashauri za Manispaa ya Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuandaa Mpango wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa.

No comments:

Post a Comment

Pages