HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 14, 2014

NDUGU ABDULRAHMAN KINANA KATIBU MKUU WA CCM AENDELEA NA ZIARA RUFIJI

1 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Juma Abeid Diwani wa Kata ya Magawa wilayani Mkuranga wakati alipotembelea shamba la Mikorosho lenye hekari 1000 ambapo mikorosho inayokaribia elfu 20 imeharibika vibaya baada ya kupata ugonjwa unaonyausha mikorosho hiyo , Diwani huyo amesema wananchi wa kata hiyo wako katika hali mbaya kwakuwa zaidi ya miaka minne sasa hawajavuna chochote na maisha yao yanazidi kuwa mabaya, Katibu Mkuu Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Pwani, Tanga na Iringa akikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- 2 
Juma Abeid Diwani wa Kata ya Magawa wilayani Mkuranga akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akikagua shamba hilo leo. 3 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwishehe Mlao jinsi mikorosho hiyo ilivyoharibika kutokana na kukumbwa na ugonjwa huo, kushoto ni Juma Abeid Diwani wa kata ya Mgama 4 
Juma Abeid Diwani wa kata ya Mgama akitoa maelezo yake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani   5 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Wilaya ya Rufiji wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili katika mji wa Ikwiriri kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu. 6 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mh. Nurdin Babu. 8 
Wajumbe wa Harmashauri kuu ya Wilaya wakiwa katika kikao cha ndani kilichofanyika kwenye ukumbi wa FDC mjini Ikwiriri 9 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Harmashauri kuu ya Wilaya.kilichofanyika kwenye ukumbi wa FDC mjini Ikwiriri10 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi  kwenye ofisi ya mafundi seremala mjini Utete.  12 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya viti kutoka kwa kikundi cha vijana Maseremala mjini Utete kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi na wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo la Rufiji na Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Dr. Seif Rashid.11 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi Ofisi ya CCM wilaya ya Utete 13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jengo la ofisi ya CCM wilaya ya Utete 14 
Mmoja wa wapiga ngoma wa kikundi cha ngoma cha mjini Utete akipiga ngoma huku akiwa amebeba mtoto wake mdogo na mtoto wake mwingine akiwa amekaa pembeni. 15 
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo. 17 
Mkuu wa wilaya ya Rufiji Mh. Nurdin Babu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Utete leo 18 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa Utete katika mkutano uliofanyika leo mjini humo 19 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi akimuwekea kipaza sauti mmoja wa wazee waliofika kwenye mkutano ili kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na kuuliza maswali yake 20 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana Utete wakati wa mkutano wa hadhara uliofnyika mjini Utete.  21 
Baadhi ya wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi wakila kiapo mara baada ya kupokea kadi zao za uanachama 23 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi wakinyanyua mikono yao juu wakati wakila kiapo cha utii kwa chama, 24 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Dr. Onesmo Mambosho Mganga Mfawidhiwa wa kituo cha afya cha Nyamwage.

No comments:

Post a Comment

Pages