HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2014

RAIS KIKWETE AWAPANDISHA VYEO MAAFISA SABA WA JWTZ

Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kushoto akimvisha cheo kipya Meja Jenerali Simon Mumwi, Makao Makuu JWTZ Upanga jijini Dar es salaam,Septemba 17,2014.


Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kushoto akimvisha cheo kipya Meja Jenerali Ndetaulwa Zakayo Makao Makuu JWTZ Upanga jijini Dar es salaam.



Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kushoto akimvisha cheo kipya Meja JeneraliVenanceMabeyo.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kushoto akimvisha cheo kipya Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Meja Jenerali James Mwakibolwa mara baada ya kuvishwa cheo kipya na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange hayupo pichani.
 
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, kwa mujibu wa Kanuniza Majeshi ya Ulinzi, Ayaya 7.01 Kifungu cha (3) amewapandisha cheo Maafisa Saba (7) kutoka Brigedia Jenerali kuwa Meja Jenerali kuanzia Septemba 12, 2014.  Waliopandishwa cheo ni kama ifuatavyo:-  

            Brigedia Jenerali Gaudence Milanzi kuwa Meja Jenerali.

             Brigedia Jenerali James Mwakibolwa kuwa Meja Jenerali.

               Brigedia Jenerali Ndetaulwa Zakayo kuwa Meja Jenerali.

              Brigedia Jenerali Venance Mabeyo kuwa Meja Jenerali.

             Brigedia Jenerali Simon Mumwi kuwa Meja Jenerali.

                Brigedia Jenerali Issa Nassor kuwa Meja Jenerali.

                Brigedia Jenerali Rogastian Laswai kuwa Meja Jenerali.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amewavisha cheo cha Meja Jenerali kwa niaba ya Rais. Sherehe hizo fupi zitafanyika Makao Makuu ya JeshiUpanga Dar es Salaam.

Aidha, Meja Jenerali Milanzi, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi waTaifa (NDC) kufuatia nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mkuuwa Chuo hicho Luteni Jenerali Charles Makakala ambaye amestaafu. Kwa mujibu wa sharia baada ya kulitumikiaTaifa kwa uaminifu na uadilifu wa hali ya juu.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963

No comments:

Post a Comment

Pages