HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 26, 2014

WARIOBA AFUNGUKA

 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akifafanua jambo kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba lilivyochakachua maoni ya wananchi wakati wa hafla ya kutimiza 19 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watetezi wa haki za binadamu wakiwa katika mkutano huo.
 Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia (kulia).
 Ndimara Tegambwage (katikati), kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
 Warioba akifafanua jambo kuhusu Bunge Maalum la Katiba.
 Wageni waalikwa.
 Warioba akifafanua jambo kuhusu Bunge Maalum la Katiba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk. Helen Kijo Bisimba (kushoto), Askofu Elinaza Sendoro na Prof. Chris Maina (kulia).
 Washiriki.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo Bisimba
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizindua kitabu cha Breathing the Constitution kilichoandikwa na Dk. Sengondo Mvungi. 
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo Bisimba, Askofu Elinaza Sendoro, na Prof. Chris Maina wakionyesha kitabu cha Breathing the Constitution kilichoandikwa na marehemu Dk. Sengondo Mvungi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo Bisimba akionyesha kitabu cha Breathing the Constitution kilichoandikwa na marehemu Dk. Sengondo Mvungi. Kulia ni Askofu Elinaza Sendoro.
 
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

MWENYEKITI  wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema  kwa hali ya mambo yanayoendelea bungeni haoni matumaini ya kupatikana kwa katiba mpya na kwamba hali hiyo imemkatisha tamaa.

Wakati jaji Warioba akikatishwa tamaa na uwezekano wa kupatikana katiba mpya, Muhadhiri wa vyuo mbali mbali nchini Profesa Chris Peter Maina, ameeleza kuwa watu wanaotaka kuzuia historia kuandikwa kwa kutumia askari wa Kutuliza ghasia hawatafanikiwa kwa kile alichoeleza kuwa historia itawaumbua watu wa aina hiyo.

Jaji warioba na Profesa Maina walitoa kauli hiyo jana jijini Dar e sSalaam wakati wa kumbu kumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki kwa Dk. Sengondo Mvungi, pamoja na hafla ya  kutimiza miaka  19 ya  kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC).

Katika matukio hayo mawili yaliyoendana na uzinduzi wa kitabu cha historia ya maisha ya  Dk Mvungi Jaji Warioba alisema, tangu mwanzo matumaini yalikuwa ni nchi kupata katiba mpya kwa maridhiano  na kwamba baada ya mchakato huo wa katiba kutekwa na wanasiasa matumaini hayo yametoweka
Alisema badala yake wanasiasa hao wameacha kuangalia maslahi ya taifa na kutegemea uamuzi wa kura badala ya nafasi ya maridhiano kupewa kipaumbele.

 “Sina hakika  kama tutapata katiba mpya kwani rasimu itakayopendekezwa na bunge maalum haitapigiwa kura hadi mwaka 2016 kwa kuwa hakuna maridhiano hasa kuhusu muungano rasimu hiyo itaanza kupigwa tangu siku ya kutolewa kwake.”alisema na kuongeza
Kampeni ya uchaguzi ya mwaka kesho katiba mpya itakuwa agenda inayoweza kuigawa nchi.

Akiongelea rasimu iliyopitishwa n a bunge maalum la katiba jaji Warioba alisema limepitisha rasimu yake na kuacha maoni yaliyotolewa na wananchi na kwamba jambo hilo ni hatari
Jaji Warioba alisema licha ya baadhi ya mambo kuonekana kukubaliwa katika rasimu hiyo ya bunge bado kuna mambo mengi ya msingi yamewekwa pembeni na kwamba wabunge waliopitisha uamuzi huo wanapaswa kutoa maelezo ya kutosha kwa wananchi
Aliyataja baadhi ya mambo ambayo mwelekeo wake ni kukataliwa  na wananchi kuwa ni pamoj.

Maadili ya viongozi 
Katika  maadili ya viongozi  alidai kuwa wananchi walitoa maoni mazito kuhusu maadili  ndani ya jamii na maadili ya viongozi kwa kuwa wanachukizwa na kuporomoka kwa maadili.

Kutokana na maoni ya wananchi, alisema Tume iliimarisha misingi  mikuu ya taifa iliyo katika utangulizi wa rasimu ambako misingi katika katiba ya sasa ni uhuru, haki udugu na amani lakini kutokana na maoni ya wananchi misingi mipya iliongozwa nayo ni pamoja na utu,usawa, umoja na mshikanamo.

Wananchi pia walipendekeza tunu za taifa ziwekwe kwenye katiba, tunzu hizo ni pamoja na utu, uzalendo, uadilifu,umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya taifa ya Kiswahili.

Hata hivyo Warioba alisema ni jambo la kusikitisha kwa kuwa Bunge maalum  limeondoa uadilifu, uzalendo, umoja, uwazi  na uwajibikaji kutoka kwenye orodha ya tunu za taifa na kuziweka kwenye misingi ya utawala bora na kuongeza kuwa kila mtanzania anapaswa awe na tunu hizo.

Madaraka ya wananchi
Kuhusu madaraka ya wananchi alisema kuwa katiba inatungwa na wananchi na kwa maoni yao wanataka wawe na madaraka ya  kumwondoa mbunge wao kama hawaridhiki na uwakilishi wake.
Akilifafanua hili alisema ni kweli siyo jambo la kawaida kumwondoa mbunge katikati ya kipindi  au kumwekea ukomo, lakini kwa sababu ya rushwa katika uchaguzi wananchi wanaona ni vema watumie madaraka yao kuwajibisha  wabunge wao.
Katika hili alisema hii inawekana kwa kuwa tayari bunge lina kanuni za kuwaajibisha wabunge, vyama vya siasa vina madaraka ya kuwaondoa vivyo hivyo wanannchi nao wanapenda kuwa na madaraka hayo.

Mgawanyo wa Madaraka kati ya mihimili
Warioba alisema pendekezo la kumwondoa Rais na Mawaziri kutoka kwenye Bunge linakataliwa kwa sababau kumezoeleka mfumo wa kibunge kama ilivyo kwa nchi za jumuiya ya madola.
“Siyo kweli kwamba mfumo wetu ni wa kibunge kwani kwenye mfumo wa kibunge mkuu wa nchi hana madaraka ya utendaji bali madaraka hayo yako mikononi mwa Waziri Mkuu ambaye ni mbunge na hivyo ndivyo ilivyo kwa Uingereza, India, Canada, Australia na New Zealand.

“Ikumbukwe kwamba  Tanzania ina mfumo wa Urais ambapo rais ni mkuu wa nchi, Mtendaji Mkuu, Amir Jeshi Mkuu hivyo Rais na Mawaziri wake kuwa sehemu ya Bunge ni kuchanganya mamlaka ambako hali hii ndio inafanya Serikali kuingilia mamlaka  ya bunge na pia bunge kuingilia mamlaka ya serikali.

“Tumeona wakati mchakato huu wa katiba jinsi madaraka yanavyoingiliana ambako wakati wa kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba tuliona jinsi bunge lilivyokuwa linafanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kutunga sheria.

“Lakini baadaye Rais anafanya mazungumzo na watu nje ya bunge na baadaye bunge linalazimika kubadili maamuzi ambako hata bunge maalum la katiba limetendewa hivyo kwa maana hiyo bunge halina madaraka kamili na Rais anaweza kuingilia wakati wowote,”alisema Warioba.

Wakati katika Bunge la kawaida alisema mawaziri wanawabana wabunge kupitisha mambo ya Serikali na wabunge mara nyingine wanaingilia kazi za Serikali kwa mfano kamati za bunge kwenda moja kwa moja kwenye taasisi za Serikali kutoa maagizo au kutoa maazimio kwa hatua kuchukuliwa kwenye maeneo ya utendaji.
Hivyo anachoona yeye dhana ya kutenganisha madaraka ya mhimili ni jambo la msingi sana katika mfumo wa demokrasia na nchi nyingi zimebadili katiba ili kutenganisha madaraka na mihimili na zimefanya hivyo na sababu zao zinafanana kabisa na zile ambazo wananchi wa Tanzania walitoa.

Muundo wa Muungano
Katika suala la muungano ambalo ndilo limeteka nafasi kubwa ya majadiliano tangu mchakato huo uanze, Warioba alisema pamoja na Tume kuorodhesha  kero zaidi ya 40, baada ya uchambuzi wa kina ilionekana kero nyingi ama zimepatiwa ufumbuzi au zinaweza kurekebishwa na tume ilichambua tu zile kero ambazo zilionekana ni nzito.

Huku akidai kuwa lalamiko kubwa kwa upande wa Tanzania Bara ni Zanzibar kuvunja katiba ya Muungano ambako alihoji kuwa kutokana na yale yaliyopitishwa na Bunge la sasa ni kweli Zanzibar itakubali sheria zanazotungwa na Bunge kutumika nchi nzima bila masharti.

Swali lingine ni kama kweli Zanzibar imekubali Mahakama ya Rufaa na Mahakama ya Juu ziwe mamlaka nchi nzima bila masharti, itakubali kuondoa mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2010 na suala la Bunge kupendekeza kwamba raia awe na haki kupata ardhi, je Zanzibar wamekubali raia wote wawe na haki hiyo kwa upande wa Zanzibar.

Awasubiri wabunge mitaani
Kuhusu Shutuma mbali mbali zilizoelekezwa na wabunge wa bunge maalum kwa wajumbe wa Tume yake, Jaji Warioba alisema baada ya wabunge hao kumaliza kuongea katika vipaza sauti vya bunge wanapaswa kutambua kuwa wanawasubiri mitaani
“Wao wanasema jaji Warioba na wajumbe wenzake ni Shiidaah tena wanasema Warioba ni shida kubwa, mimi nawaambiua wanakaribia kuacha vipaza sauti vya bunge waje huku mitaani wawaeleze wananchi yale waliyopitisha na sisi tutabaki katika msimamo wa kutetea maoni ya wananchi hapo ndipo watakapojia kama walio na shida ni sisi au wao”alisema Warioba

No comments:

Post a Comment

Pages