HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 21, 2014

WATANZANIA MSIWACHAGUE VIONGOZI WENYE UCHU WA MADARAKA

Na Mwandishi Wetu

ASKOFU wa Kanisa la Hossana Life Mission Ephraim Mwansasu, amewataka Watanzania kutowachagua wanasiasa ambao wako tayari kumwaga damu ili mradi wapate madaraka katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa ibada ya kuliombea Taifa, iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Askofu Mwansasu, alisema kuna ishara ambazo zinaashiria kuvurugika amani.

Alisema ili kuepuka kuvurugika kwa amani na kumwaga damu nchini ni vema Watanzania wakajiandaa kuchagua viongozi ambao hawako tayari kuona damu ina mwagika.

“Mwanasiasa yeyote anayenuia mabaya tusimkubali hata itikadi anayosema madhali anakusudia mabaya tunaenda kuwashusha kwa jina la bwana,”alisema Askofu Mwansasu.

Askofu, alisema wako tayari kumuombea kiongozi yeyote, ambaye anaonesha nia ya kudumisha amani, umoja na kupigania haki za wanyonge, ili awezekuchaguliwa hata kama hana uwezo wa kifedha.

Akizungumzia ishara nyingine ambazo zinaweza kuliingiza taifa katika mifarakano ni vitendo vya polisi kuingia kwnye  migogoro na wandishi wa habari.

Askofu Mwansasu, alisema kitendo cha kupigwa wandishi wahabari ni jambo la hatari ambalo linaweza kuliingiza taifa katika machafuko yasiyotarajiwa.

“Ufike wakati vyombo hivi muhimu ambavyo vinategemeana sana katika majukumu yao ya kila siku, hivyo ni vema vikaheshimiana ili kila kimoja kijiamini kwa mwenzake”alisema Askofu Mwansasu.

Aliongeza kwa kusema kuwa hata matabaka yanayojitokeza katika vyama vya siasa vikiwemo vikubwa na vidogo, nayo pia yanatishia kuvurugika kwa amani, yote hayo yanapaswa kuombewa ili vyama hivyo viweze kuwa na mshikamano kwa ajili ya kuzalisha viongozi bora.

No comments:

Post a Comment

Pages