HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 29, 2014

Mchungaji TAG; Muungano wa UKAWA Ulingojewa!

Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakionesha hati za waraka walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Na Bryceson Mathias, Morogoro

MCHUNGAJI wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Mazimbu Morogoro, James Power Mabula, amesema, Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ndio hasa uliongojewa na Wananchi.

Mabula ambaye ni Muumini wa Serikali Tatu alisema, wanaobeza wakubali wasikubali, kuwepo kwa Muungano wa UKAWA ndiko hasa kulikongojewa na Wananchi walio wengi.

“Pamoja na kwamba kutakuwepo na akina, Yuda Iskariote, waliotumwa na Farao, ili kumuua UKAWA, hata wao watabaki na nguo wakishangaa kama Askari wa Kiyahudi walivyobaki na Sanda, Yesu akiwa amefufuka, na wakawa wa kwanza kusema amefufuka..

“Hakuna ubishi baada ya wananchi wengi wanaopenda mabadiliko kuwa na kigugumizi nani wamchague katika chaguzi mbalimbali kati ya wagombea wengi wa upinzani, makubaliano ya Muungano wa UKAWA uliofanyika hivi karibuni, umetoa Jibu nini kifanyike”alisema Manula.

Alinukuu Yoshua 7:1 ‘Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana wa Israeli.

Mabula alishangazwa na kuwahoji, baadhi ya wajumbe waliokuwa kwenye Bunge Maalum la Katiba wakijiita Viongozi wa Dini, waliomtumikia Mungu kwa miaka mingi, akisema Mbona walisema Uongo?

Aliuliza, Watasemaje Viongozi wa dini hao hao wasema Marehemu kapiga kura? Watasemaje Mtu wa Bara apige kura Z’bar? Alihoji Je, Wanajua maandiko katika Biblia Zaburi 5:6? Mungu aliulizwa, “Utawaharibu wasemao Uongo; Bwana humzira Mwuaji na mwenye Hila?”.

Aliwaasa Ukawa akisema, wao kama Yoshua wa leo, Mtu akisema, “Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake. Aitwe Bonde la Akori”

No comments:

Post a Comment

Pages