HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 01, 2014

MICHUANO YA WAZI GOFU OKTOBA 4

 Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya UAP Insurance, Raymond Komanga akifafanua jambo wakati wa akitangaza mashindano ya gofu yaliyoandaliwa na kampuni hiyo yatakayofanyika Oktoba 4 jijini Arusha. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Uendeshaji wa UAP Insurance, Michael Kiruti na Meneja Uandikishaji Bima,  Ally Athuman. (Picha na Francis Dande)

Na Mwandishi Wetu

Mashindano ya wazi ya gofu ya Arusha gofu championships yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 4 mwaka huu katika uwanja wa Gymkhana jijini Arusha.

UAP ambao ni kampuni la huduma ya utoaji Bima, uwekezaji na utawala, uwekezaji wa vitega uchumi na maendeleo, pamoja na kuwa washauri katika mambo ya fedha na ulinzi wa mali, ndio waandaaji wa mchuano huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam Meneja Biashara wa Kampuni ya UAP Insurance Tanzania inayoratibu michuano hiyo Raymond Komanga alisema wanatarajia kushirikisha wachezaji wa gofu wa rika zote kutoka jijini humo na hata maeneo mengine ya jirani

Komanga alisema lengo la michuano hiyo ni pamoja na kuwashukuru wakazi wa jiji la Arusha kutokana na ushirkiano wao na kampuni hiyo.

Wachezaji watakaojitokeza kushiriki katika mashindano haya watanufaika kutokana na kwamba watakuza vipaji vyao, kujenga afya pamoja na kukuza wigo wao wa washiriki wa kibiashara kupitia mchezo wa gofu, hivyo tunaomba wachezaji gofu wajitokeze siku hiyo.

Kwa sasa UAP inafanya kazi katika nchi 6 Afrikazikiwemo Kenya, Uganda, South Sudan, Rwanda, DRC na Tanzania. Baadhi ya bidhaa na huduma za UAP ni pamoja na Bima ya mazao , Bima Mifugo , Bima ya magari, Bima ya mabasi na lori , Bima ya Ndani, bima ya matibabu, bima shule , dhima ya umma , bima ya ajali ya makundi au binafsi , bima yamoto na hatarizingine na mengine zaidi.

Komanga alisema lengo lingine ni kutaka kuona michuano hiyo inapata washiriki wengi ili kutoa ushindani na kwamba huo ni mwanzo kwani bado watandaa michuano mingine.

Tutahakikisha  tunaandaa michezo  mbalimbali  ikiwemo huu wa gofu na ipo lingine  la kuandaa jijini Arusha ni kuhakikisha inakuwa na wachezji wengi wazuri  mchezo huo ambao baadaye wataweza kuichezea timu ya taifa na klabu mbalimbali8 alisema.

Alisema mshindi wa kwanza katika michuano hiyo atapata zawadi ya kulipiwa bima ya nyumba anayoishi pamoja na watu wawili anaoishi nao pili atalipiwa bima ya gofu kwa mwaka mmoja wakati mshindi wa tatu atalipiwa bima ya ajali ya aina yoyote ndani ya mwaka.

No comments:

Post a Comment

Pages