HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 01, 2014

Warembo Redd’s Miss Tanzania watamba

Na Mwandishi Wetu
 
HUKU Redds Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanya, akikiri shindano hilo mwaka huu litakuwa gumu, warembo wanaoshiriki msimu huu wametamba kufanya kweli.
 
Baadhi ya warembo hao ni Redd’s Miss Top Model, Jihan Dimachk na Redd’s Miss Photogenic, Evelyn Baasa.
 
Jihan kwa sasa amefanikiwa kuingia hatuaya nusu fainali baada ya kulitwaa taji hilo, kama ilivyo kwa Evelyn.
 
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, warembo hao walisema kushinda mataji hayo kumewafanya wazidi kujiamini zaidi na wana uhakika watafanya kweli katika shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba.
 
“Kwangu naliona taji hili hapa, nina uhakika mkubwa sasa wa kutwaa taji la Redd’s Miss Tanzania, wala sina hofu na mshiriki yoyote yule,” alisema Jihan.
 
Evelyn naye alisema; “Tayari njia ya kutwaa taji la Redd’s Miss Tanzania imefunguka. Ni kiasi cha muda tu ndio utakaothibitisha hilo.”
 
Naye Happiness alisema, amefurahishwa mno na warembo waliopo na ana uhakika mkubwa wote wana vigezo vya kulitwaa taji hilo.
 
“Warembo wote 30 wana vigezo vya kulitwaa taji hilo, maana wana sifa zote na mwaka huu kuna ushindani mkubwa zaidi,” alisema Happiness.
 
Redd’s Miss Tanzania ni shindano ambalo linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment

Pages