HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 25, 2014

ABAJALO YAINGIA FAINALI DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUPKWA KISHINDO

Timu ya Abajalo ya Sinza jijini Dar es Salaam imefanikiwa kukata tiketi ya fainali ya Dk. Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 baada ya kuifunga Burudani FC ya Temeke mikoroshini mabao 3-1. 

Mabao ya Abajalo kwenye mchezo huo yalifungwa na Idd Kulachi ‘Kleberson’ aliyefunga mabao mawili kati ya matatu. Mchezo huo wa nusu fainali ya pili ulipigwa kwenye uwanja Bandari uliopo maeneo ya Tandika Mwembe Yanga.

 Kwa ushindi huo sasa Abajalo itacheza na Tabata FC kwenye fainali itakayopigwa siku ya jumapili ya tarehe 30/11/2014 pale pale kwenye uwanja wa Bandari,huku timu za Black Six ya Buguruni na Burudani zikipambana kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo iliyovutia mashabiki kibao mpaka sasa,Bingwa mwa mashindano hayo atapata pesa taslim shilingi milioni tano huku mshindi wa pili akipata milioni tatu na mshindi wa tatu akiambulia shilingi milioni mbili. Capture 7 7 8 5 1 2 4 8AJALO

No comments:

Post a Comment

Pages