HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2014

ABDULRAHMAN KINANA: MUDA WA KULINDANA HAUPO TENA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika uwanja wa michezo wa Ilulu mjini Lindi wakati akihitimisha ziara yake mkoani humo leo kabla ya kuendelea na ziara mkoani Mtwara kesho. Kinana amesema viongozi wanatakiwa kuwa waadilifu na wanaojituma kuwatumikia wananchi, akaongeza kwamba muda wa kulindana haupo tena na kiongozi akiharibu awajibike mwenyewe kwa makosa yake na ni muhimu kiongozi akiingia madarakani ajue na wakati wa kutoka. Wakati huohuo  Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema katika sakata la ESCROW kila mtu aliyehusika abebe msalaba wake.Nape alisema CCM haijabadili msimamo wake ambapo alifafanua kama katika sakata la Richmond Waziri Mkuu alijiuzulu , hivyo hata kwenye ESCROW atakayebainika kuhusika naye achukuliwe hatua.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa hadharawakati akimkaribisha Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akinukuu baadhi ya vifungu vya katiba mpya inayopendekea wakati alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kwa wananchi kuhusu katiba hiyo
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo katika mkutano huo wa hadhara.
 Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano huo
 Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo ukisubiri kuanza kwa mkutano.
 Baadhi ya vijana wa chuo cha VETA wakionyesha kadi zao za umoja wa Vijana wa CCM UVCCM katika mkutano huo.
 Moja ya vikundi kikitumbuiza katika mkutano huo
 wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ilulu mjini Lindi.
Nape Nnauye akiwasili katika mkutano huo.
 Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijumuika na wanachama wa CCM kutoka Tawi la Magogoni/Rahaleo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa mafundi bati wakati walipokuwa wakipaua jengo la umoja wa vikundi vya akina mama washonaji nguo..
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia nyavu za kuvulia samaki wakati alipokitembelea mradi wa kuvua samaki huko Jamhuri Machole.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa munyumba ya mwalimu shule ya msingi Nanyenje mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la mihogo la kikundi cha kuzalisha mbegu bora za muhogo.
Muhogo wenyewe ndiyo huu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba mtari wa kilimo cha umwagiliaji mbogamboga Mingoyo Mnazi Mmjoa.

No comments:

Post a Comment

Pages