HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 20, 2014

Benki ya Exim yapanda miti na kutoa msaada wa chakula kituo cha wazee Moshi

Meneja wa Benki ya Exim wa Tawi Moshi mkoani Kilimanjaro, Bw. John Ngowi akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika baada ya benki hiyo kutembelea kituo cha Wazee cha Njoro katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Mbali na kupanda miti, benki pia ilitoa msaada wa chakula katika kituo hicho. Wakishuhudia ni wafanyakazi wa Benki ya Exim jijini Moshi.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Moshi, Kilimanjaro wakimshuhudia mmoja kati ya wanajamii wa Njoro akishiriki katika zoezi la upandaji miti lililofanywa na Benki hiyo baada ya kutembelea kituo cha Wazee cha Njoro katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Mbali na kupanda miti, benki pia ilitoa msaada wa chakula katika kituo hicho.


Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Moshi, Kilimanjaro wakimshuhudia mmoja kati ya wanajamii wa Njoro akishiriki katika zoezi la upandaji miti lililofanywa na Benki hiyo baada ya kutembelea kituo cha Wazee cha Njoro katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Mbali na kupanda miti, benki pia ilitoa msaada wa chakula katika kituo hicho.
 
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Benki ya Exim Tanzania imepanda miti mia moja kuzunguka eneo la kituo cha wazee wasiojiweza cha Njoro jijini Moshi, hatua iliyofikiwa kutokana na jitihada za Benki hiyo za uboreshaji mazingira kupitia mpango ujulikanao kama ‘go-green’ ambao umelenga kuziunga mkono jitihada za serikali nchi nzima katika utunzaji wa mazingira.

Benki pia katika tukio hilo ilitoa msaada wa chakula katika kituo hicho cha wazee. Mchango huo ukiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo za kijamii.  

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Meneja Mkuu wa Tawi la Benki ya Exim Moshi, Bw. John Ngowi alisema utunzaji mazingira ni sehemu ya jitihada za Benki katika shughuli za kijamii ambazo uendana na mpango wa benki wa ‘Go – Green’ ambao umelenga kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kulinda uhalibifu wa mazingira.

Alisema kuwa miti hiyo mia moja iliyopandwa ikitunzwa vizuri itawawezesha wazee katika kituo hicho kuwa na mazingira mazuri na hali ya hewa safi. Aliongeza kuwa mbali na zoezi hilo la upandaji miti, Benki pia imechangia chakula katika kituo ili kuwasaidia wazee katika mahitaji yao muhimu, hatua ambayo ni sehemu ya shughuli za kijamii ya benki hiyo.

 “Katika Benki ya Exim tunazitazama shughuli za kijamii kama uwekezaji katika jamii, ambao utiliwa mkazo na kanuni ya ‘Kurudisha Kile Tulichonacho kwa Jamii’. Jitihada katika shughuli za Benki za kijamii zimejikita katika maeneo makuu manne ambayo ni: Mazingira; Elimu; Afya; na Maendeleo ya Michezo,” alisema Bw. Ngowi.

Bw. Ngowi alisema kuwa dhamira za benki haijikiti pekee katika kuongeza mizania ya benki lakini pia kuhakikisha inarudisha kile ikipatacho kwa jamii ambayo inaizunguka.   

“Kupitia mwendelezo wa jitihada zilizoonyeshwa na wafanyakazi wa Benki ya Exim na menejimenti yake, tunaamini kuwa benki yetu itatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii nchi nzima.

 “Natumai mchango wetu katika kituo hichi cha wazee utakuwa na manufaa makubwa baadae. Uzoefu huu hautukumbushi tu kuwa ni muhimu kutoa kile tulichonacho kwa jamii lakini pia inatufundisha kufanyakazi kwapamoja kama timu,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages