HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 21, 2014

MAMIA WAMUAGA MWANDISHI WA HABARI WA NEW HABARI 2006 LTD, MAREHEMU INNOCENT MUNYUKU, YANGA YATOA UBANI WA 500,000

Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Innocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Innocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Mwandishi wa habari wa gazeti la Hoja, Iche Mang'enya akitoa heshima za mwisho.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa New habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa heshima za mwisho. Kushoto Mwandishi wa habari wa gazeti la Hoja, Iche Mang'enya akitoa heshima za mwisho.
 Matinyi akisoma wasifu wa marehemu.
 Mwakilishi wa klabu ya Yanga, Said Motisha akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya klabu yake ambapo alitoa ubani wa sh. laki tano.
 Motisha akikabidhi ubani wa sh. laki tano.
 Mmoja wa watu waliosoma na marehemu Munyuku akitia salama za rambirambi ambapo walitoa sh. laki tatu.
  Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando akitoa salama za rambirambi.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa salam za rambirambi.
 Mwakilishi wa familia, Mkuchika akitoa neno la shukrani.
 Rashid Kejo akitoa salama za rambirambi.
 Mwakilishi wa Uhuru Publishers akitoa salama za rambirambi na ubani wa sh. laki mbili.
 Waombolezaji wakielekea katika gari kwa ajili ya safari ya Morogoro kwa mazishi ya marehemu Innocent Munyuku.
 Mwili wa marehemu Munyuku ukiingizwa katika gari tayari kwa safari ya kwenda mkoani Morogoro kwa mazishi.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd wakiwa katika hospitali ya Lugalo wakati wa kuaga mwili wa marehemu Innocent Munyuku.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hospitali ya Lugalo wakati wa kuaga mwili wa Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, marehemu Innocent Munyuku.
 Mwandishi wa gazeti la Jamhuri, Alfred Lucas (kushoto) na Limonga Justine Limonga wa Radio Uhuru.
 Waombolezaji.
 Msanifu Mkuu wa Kurasa wa gazeti la Tanzania Daima, Emily Maya akimpa pole Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda.
Mkurugenzi wa Global Publisher, Eric Shigongo akiteta jambo na Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda. 

Na Mwandishi wetu


KLABU ya soka ya Yanga ya jijini Dar es Salaam,  imeungana na wadau mbalimbali katika kumuaga aliyekuwa mwandishi wa Habari, Innocent Munyuku,  sambamba na kutoa ubani wa sh 500,000.


Halfa hiyo ya kuaga mwili wa marehemu, ilifanyika leo jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo huku mamia wakijitokeza wakiwemo ndugu na jamaa pamoja na wandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ambapo walitoa heshima zao za  mwisho za kuaga mwili huo ambao unatarajiwa kuzikwa kesho Mkoani Morogoro.



Mbali na kuaga mwili huo, wadau mbalimbali walitoa lambilambi kwa marehemu ikiwemo klabu ya Yanga, iliyotoa ubani wa sh 500,000. 

Yanga ilitioa ubani huo kupitia kwa mwakilishi wake, Said Motisha aliyetoa kiasi hicho kwa niaba ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji.


Mbali na Yanga, wengine waliotoa ubani wao ni pamoja na kampuni ya Exusive Solution waliotoa sh laki 2, Uhuru Publishers, laki 2,  shule ya Biwana sh laki 2, na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment

Pages