HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 28, 2014

TPHA kuja na jengo la kisasa la kuinua mapato yake

Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga akiwa na wajumbe wa TPHA, akiwemo Dk. Anna Nswilla (Treasure of TPHA), (katikati) akifuatiwa na Dk.Faustine Njau (TPHA Life Member).
Na Andrew Chale, Bagamoyo
CHAMA Cha Afya ya Jamii Tanzania (Tanzania Public Health Association-TPHA), kipo kwenye mkakati kabambe wa kuendeleza na kuinua mapato ya chama hicho ikiwemo kujenga jengo la kitega uchumi la kisasa litakalo kuwa na zaidi ya gorofa 20, katika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam. 
Hayo yalibainishwa mjini hapa kwenye kongamano la 31 la Kisayansi naMkutano mkuu wa mwaka wa TPHA unaoendelea katika ukumbi wa Stella Maris, mjini Bagamoyo ambapo wataalamu wa majengo nchini wa kampuni ya K&M Archplans (T)Ltd, walipowasilisha mpango kazi wao huo ikiwemo mchoro wa jengo hilo la TPHA litakavyokuwa.
Wataalamuhao wa K&M Archplans, kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Profesa Arch Livin Mosha alisema kampuni yao imebobea katika ukandarasi wa majengo mbalimbali ikiwemo kuwa na uzoefu wa kutosha katika usanifu na mpanilio wa majengo.
Jengo hilo linatarajiwa kujengwa makao makuu ya TPHA, yaliyopo Kinondoni, Victoria Makumbusho, jijini Dar es Salaam.
Naye Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe alieleza kuwa, Chama hicho kitaendela na mchakato wake ikiwemo kujadiliana kwa kina na wanachama katika kufikia malengo ya utekelezaji wake ambapo mpango wa TPHA kuwa na jengo la kisasa la gorofa 10 ama 25 ambapo itategemea na mchakato wake.
NayeKatibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano hilo ni la kuwakutanisha wataalamu ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutoa mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii hususani sekta ya afya hapa nchini.
Kongamano hilo la kisayansi lililoanza Jumatatu ya Novemba 24, wiki hii, linatarajia kumalizika Ijumaa ya Novemba 28 wiki hii.

No comments:

Post a Comment

Pages