HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 07, 2014

ANGLICANA TANGA WAANZISHA MFUKO WA MAFUO YA UZEENI KWA WATUMISHI WAKE

KANISA la Anglicana Dayosisi ya Tanga limeanzisha mfuko wa kulipa malipo ya uzeeni (Pensheni), watumishi wake kama mafao yatakayowasidia baada ya kustaafu
utumishi katika kanisa hilo.

Hayo yalisemwa na Askofu wa kanisa hilo Mahimbo Mndolwa wakati alipokuwa akizungumza kuhusu sherehe ya kumuaga mchungaji wa kigango cha Mashewa Thomas Ngereza, iliofanyika  katika Kanisa ST. Andrews Manundu wilayani Korogwe Mwishoni mwa wiki.

Askofu Mndolwa, alisema kuanzishwa kwa mafao hayo ya uzeeni kutasaidia mhusika wakati atakapostaafu aepukane na maisha magumu yatakayowafanya wageuke kuwa ombaomba.

“Leo kwa pamoja tukiongozwa na Mwenyekiti wetu Dominic Singano tumemzawadia mstaafu mabati 59, mbao, misumali kilo 10 pia alikabidhiwa cheti,”alisema Mndolwa.

Askofu Mndolwa, aliyataja baadhi ya mafao ambayo atayopatiwa mstaafu ni kama vile nyumba, gari na fedha, ambayo anaamini kuwa yatamsaidia mstaafu huyo katika kupambana na changamoto mbalimbali za maisha.

Licha ya kumuaga mchungaji Ngereza pia walikuwepo watumishi wengine wanne  waliostaafu kutoka katika Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi ya St. Agustino  ya wilayani Muheza  ambao ni Mery Dismasi,Charles Juma, Peter Rajabu na Itikija Mbaga.

Askofu mstaafu wa Aglicana Dayosisi ya
Tanga Philip Baji, alikemea tabia za baadhi ya wachungaji ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa
sadaka.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Askofu  mkuu mstaafu Anglicana Verentino Mokiwa kutoka jijini Dar, Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Zanzibar Michael Afizi na  Padri Joseph Mhina.

No comments:

Post a Comment

Pages