HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 19, 2014

Beach Band Bonanza kutikisa ufukweni Kesho

Rais wa Band ya FM Academia, Nyoshi El Saadat akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu tamasha la burudani liitwalo 'Beach Band Bonanza' litakalofanyika kesho Jumamosi katika Ufukwe wa Azura, Kawe jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Biashara wa Kampuni ya Mabibo Beer inayodhamini bonanza hilo kupitia kinywaji cha Windhoek, Joseph Boniface.
Na Mwandishi Wetu
 
BENDI mbalimbali za muziki wa dansi na wasanii wa Bongo Fleva wanatarajia kushiriki katika bonanza la burudani liitwalo ‘Beach Band Bonanza’ litakalofanyika Desemba 20 katika Ufukwe wa Azura, uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa ‘Team Mamba’ ambao ni waratibu wa bonanza hilo, Doris Godfrey alisema bonanza hilo litashirikisha bendi kama FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma,’ Skylight, Mapacha Watatu, wasanii wa Bongo Fleva, akiwemo Dully Sykes, CPWAA na Yamoto Band.

“Napenda kuwakaribisha katika bonanza hili, tutachanganya ladha tofauti ili kuvutia kwa kujumuisha Bongo Fleva na Dansi, kiingilio kitakuwa Sh 10,000 na watoto Sh 5,000, tunatarajia kuanza saa sita mchana na pia kutakuwa na michezo mbalimnbali ya watoto,” alisema.

Meneja Biashara wa Kampuni ya Mabibo Beer inayodhamini bonanza kupitia kinywaji cha Windhoek, Joseph Boniface, alisema bonanza hilo ni la aina yake na wao wameamua kuzikutanisha bendi za muziki wa Dansi na Bongo Fleva kuwapa burudani mashabiki.
                    

No comments:

Post a Comment

Pages