HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 20, 2014

COASTAL UNION KUKIPIGA NA MOMBASA COMBAIN KESHO NCHINI KENYA

NA MWANDISHI WETU, TANGA

 TIMU ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya”wanatarajia kusafiriki kuelekea nchini Kenya kesho kucheza mechi ya Kirafiki na Mombasa Combaini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa soka Manispaa ya Mombasa ambao unaatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na joto lililopo mjini Mombasa kuelekea mechi hiyo.

Akizungumza leo, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kinachosubiriwa ni siku ya mechi hiyo ambayo ni kesho.

Assenga amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ni kipimo tosha kwa Kocha Mpya wa timu hiyo, James Nandwa kuangalia kiwango cha timu hiyo kabla ya kuwavaa wapinzani wao Tanzania Prison.

Hata hiyo amesema kuwa  licha ya kocha huyo kuangalia kiwango cha wachezaji ambapo mechi hiyo itakuwa ni ya pili kusimama kwenye bechi ya kwanza ilikuwa ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui ya Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

Pages