HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 14, 2014

MAMIA WAJITOKEZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 Wakazi wa Mtaa wa Makangira Msasani wakiwa katika foleni ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchi nzima leo.
Wakazi wa Mtaa wa Makangira wakihakiki majina yao.
Wakazi wa Mtaa wa Makangira wakihakiki majina yao.
Wapiga kura wakipiga kura.
Foleni ya kupiga kura.
Mzee Focus Stevin akipiga kura za kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Makangira jijini Dar es Salaam leo asubuhi.


Mmoja wa wapiga kura waliojitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Darajani, Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro akiwa kwenye foleni huku akiwa amembeba mtoto. (Picha na Dixon Busagaga)


Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akizungumza na waandishi wa habari katika Kata ya Mwangata juu ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na changamoto zilizojitokeza hususan ucheleweshaji wa fomu za upigaji kura kwa baadhi ya vituo. (Picha na Denis Mlowe)


Mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam akipiga kura katika Kituo cha Omari Omari kilichopo katika Mtaa wa Maganga. (Picha na Francis Dande)


Kituo cha kupiga kura kilichopo Mtaa wa Kinondoni Mjini kikiwa kimefungwa baada ya kutokea vurugu kubwa na kusababisha kusitishwa kwa zoezi hilo. (Picha na Francis Dande)


Mawakala wa Vyama vya Siasa kwenye Kituo cha Jangwani, Monduli, mkoani Arusha wakiwa wamebeba maboksi ya kura wakielekea kituo cha Shule ya Msingi Jangwani kwa ajili ya kuhesabu, baada ya kugoma maboksi hayo kubebwa na gari ya Halmashauri kwa kuhofia uchakachuaji. (Picha na Grace Macha)

No comments:

Post a Comment

Pages