HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 03, 2014

MWANAMKE AJIFUNGUA WATOTO 11 INDIA

Mwanamke wa India katika kile kinachoonekana kuwa maajabu ya dunia ya aina yake kuwahi kutokea duniani amefanikiwa kujifungua salama watoto wafuatao 11 (kumi na moja) kwa mara moja, jambo ambalo wauguzi na madaktari wote bingwa  hawajawahi kuliona popote pale Hospitalini walipowahi kutoa huduma kwa wajawazito,bali hata kwa hospitali zote za dunia hakujawahi kusikika kitu cha namna hiyo. 

Picha ya mama huyu akiwa na watoto wake 11 imeutikisa mtandao wa Internet na kufanikiwa kujichukulia headline katika magazeti mbali mbali ya dunia ya kila siku, ikiwa na anuani ifuatayo:

"Mwanamke wa Kihindi ajifungua Timu ya Taifa yenye jumla ya wachezaji 11".

Vyanzo vya Habari vya India vimesema kwamba:Mama huyo aliyetajwa anatoka  katika familia ya kimaskini na amejaribu kuelekea katika moja ya Hospitali za umma za Serikali ya India ili kujifungua,na mumewe ni mfanyakazi katika  moja ya maduka ya Ubani (au Uvumba).

Vyanzo vimeongeza kuwa:Timu ya  madaktari imeshangaa sana, na kilichowashangaza zaidi ni ule ukubwa wa tumbo la mama mjamzito ambao hauendani sawa na urefu wake pamoja na ukubwa wa mwili wake,na kwamba kuzaliwa  watoto idadi hii kumewaacha midomo wazi wasimamizi,wauguzi,madaktari,na utawala mzima wa hospitali,bali hata kila aliyekuwepo katika Hospitali hiyo wakiwemo wagonjwa na wale walio zimia na kupoteza fahamu,nao wameshangaa.

Hospitali hiyo  ghafla imejikuta ikigeuka kuwa sehemu ya kivutio kwa wale walio miminika mahala hapo ili kushangaa shangaa na kutizama watoto hao mapacha 11 waliotimia maguu duniani.

No comments:

Post a Comment

Pages