HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 20, 2014

SIMBA YAENDELEA KUTOA VIPIGO, YAICHAPA MWADUI YA SHINYANGA 3-1

 Fair Play.
Timu za Simba na Mwadui Utd zikiingia uwanjani wakati wa mchezo wa kirafiki iliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. (Picha na Francis Dande)
 Kocha wa Mwadui Utd, Jamhuri Kihwelu (kulia) akiwa na Kocha Msaidizi Amri Said 'Stam' (katikati) wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 3-1.
 Kikosi cha Simba.
Benchi la ufundi la Simba.
Mashabiki waliofika uwanjani.
Benchi la ufundi la Mwadui.
 Kikosi cha Mwadui Utd.
Beki wa Simba, Mohamed Hussein akimtoka mshambuliaji wa Mwadui Utd, Salim Khamis wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Ahmed Mkweche akimtoka mchezaji wa Simba.
Kipa wa Simba Ivo Mapunda akiokoa moja moja ya hatari langoni mwake huku akizongwa na mshambuliaji wa Mwadui Utd, Uhuru Selemani.
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
Wachezaji wa Mwadui Utd wakishangilia bao lao la kufutia machozi.
Wachezaji wa Simba wakitoka mapumziko.

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya soka ya Simba leo imewatandika bakora 3-1 Mwadui Utd inayofundishwa na Kocha aliyewahi kuifundisha Simba, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, kwa kuwabandika mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo iliyokuwa yenye msisimko mkubwa kutokana na Mwadui Utd kuundwa na nyota kadhaa waliowahi kung'ara wakati wakizichezea timu kubwa akiwemo Athuman Idd ‘Chuji,’ Uhuru Selemani na Razak Khalfan, Ahmed Mkweche na Julius Mrope.

Mbali ya nyota hao waliopangwa kikosi cha kwanza cha Mwadui, nyota wengine mahiri kama Juma Jabu na BakarKigodeko, walikuwa katika benchi, hivyo kuongeza mvuto wa mechi hiyo licha ya tofauti ya madaraja ya timu hizo.

Dakika ya 10, Simba walikuwa wa kwanza kufika katika lango la Mwadui Utd, mpira uliopigwa na Iddy Bahati kutoka kushoto mwa lango na kukosa mmaliziaji.

Dakika ya 22, Simba walifika kwa mara ya pili katika lango la Mwadui, lakini Ibrahim Ajibu alishindwa kuitendea haki krosi-pasi murua ya Hassan Kessy aliyetua Msimbazi kupitia usajili wa dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro.  

Dakika ya 26, Simba walipata bao la kwanza likifungwa na Ibrahim Ajibu kabla ya vijana wa Mwadui Utd kucharuka na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 30, likifungwa na Salim Hamis. 

Simba walizidi kulisakama lango la Mwadui Utd na kufanikiwa kupata bao la pili dakika 37, likifumgwa kwa mara nyingine na Ajibu, hivyo Simba kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili kiliendelea kuwa cha mashambulizi kwa kila upande, lakini Simba wakionekana wametulia zaidi na kufanikiwa kupata bao la tatu likifungwa na Yusufu Mbaraka akipokea pasi kutoka kwa beki mahiri Kessy aliyekuwa mwiba mkali akipanda na kushuka.

No comments:

Post a Comment

Pages