HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 28, 2015

LIPUMBA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Prof. Lipumba akiingia Mahakamani leo mchana.
Prof. Lipuimba akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi wakati akiingia mahakamani leo.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya Kituo Kikuu cha Kati.
Doria.
Prof. Lipumba akitoka Kituo cha Polisi cha Centre.
Polisi wakiwa wamemuwekea ulinzi Prof. Lipumba ndani ya chumba cha mahakama. 
Wafuasi wa CUF wakiwa nje ya Mahakama.
Lipumba akiwa kizimbani.
Lipumba akitoka mahakamani
 Haki..................
Lipumba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata dhamana.

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, leo amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa nashitaka la jinai kwa kuwashawishi wafuasi wake kufanya fujo.

Lipumba alifikishwa kwenye viwanja vya Mahakama hiyo majira ya saa saba mchana, akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi, waliombatana na wafuasi wa chama hicho.

Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Isaya Alfani, wakili wa Serikali, Joseph Maugo akisaidiana na Hellen Mushi, alidai kwamba shauri hilo ni jipya na mshitakiwa anakabiliwa na shitaka moja.

Wakili Mauogo alidai kuwa mshitakiwa anakabiliwa na shitaka la mkuwashawishi wafuasi wake kutenda makosa ya jinai kati ya Januari 22 na 27 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam.

Alidai kwamba katika siku hizo tofauti, akiwa kama Mwenyekiti wa CUF alishawishi wafuasi wake kutenda makosa hayo, ikiwa ni kinyume cha sheria 390 na 30 ya Sheria ya kanuni ya adhabu.
Baada ya kusomewa shitaka hilo, Hakimu Alfani alimuuliza mshitakiwa kama anakubaliana na kosa hilo, lakini mtuhumiwa alikana na kusema ni uongo kabisa wala hakuhusika.

Hata hivyo, wakili Maugo alidai kwamba upande wa utetezi hauna pingamizi kuhusu mshitakiwa kuwekewa dhamana, pia upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo anaomba kupangiwa tarehe kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo.

Baada ya kutoa madai hayo, upande wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili watano, Peter Kibata, Mohammed Tibayendera, John Malya na Fredrick Kiwelo walikili kusikia maelezo aliyosomewa mshitakiwa huyo.

Wakili Kibatala aliiomba mahakama iweze kutoa masharti ya dhamana ambayo ni madogo, kutokana na mshitakiwa huyo kufahamika kama ni Mwenyekiti wa CUF, pia ni muamifu.

Hakimu Alfani alisema kuwa mahakama haina pingamizi katika maombi hayo, hivyo alimtaka mshitakiwa ajiwekee dhamana ya shilingi milioni mbili, pamoja na wadhamini wawili waaminifu watakaotoa kiasi hicho kwa kila mmoja.

Hata hivyo, Hakimu Alfani alimuachia Lipumba kwa dhamana baada ya kukidhi masharti hayo, ambapo aliahirisha shauri hilo hadi Februari 26, mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
Waliojitokeza kumdhamini Mwenyekiti huyo ni Diwani wa Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam, Ilda Aman pamoja na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Kuruthum Mchuchuli.

Baada ya kupata dhamana, akiwa nje ya Mahakama Lipumba alisema kwamba nchi ya Tanzania haina haki wala sheria kwani kesi iliyompeleka Mahakamani hapo amebambikiziwa.

"Hawa jamaaa hawana nia njema na sisi, hapo walipo wanamipango ya kuumiza watu wengine, hivyo inatakiwa tutawanyike turudi makwetu hadi tutapokutana kwenye mkutano wa adhara siku ya Jumapili kwenye viwanja vya Manzese,"alisema Lipumba.

1 comment:

  1. Wow that was unusual. I just wrote an very long comment but after I clicked submit my comment didn't show
    up. Grrrr... well I'm not writing all that over again. Anyway,
    just wanted to say fantastic blog!

    Feel free to visit my homepage: home improvement renovation ()

    ReplyDelete

Pages