HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 29, 2015

WAFUASI 30 WA CUF WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Baadhi ya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wanaotuhumiwa kuandamana bila kibali Januari 27 wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)
 Wakili wa washtakiwa John Malya akipeana mkono na Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya mahakamani hapo. 
 Askari wa upelelezi (kushoto) akiwa mbele ya watuhumiwa.
Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wanaotuhumiwa kuandamana bila kibali Januari 27 wakipanda basi la Magereza baada ya kukosa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. 
 Watuhumiwa wakiwa ndani ya basi la Magereza.
 Askari Polisi wakiwa wameimariusha ulinzi mahakamani
 Askari Polisi akiwa nje ya mahakama.


Na Mwandishi Wetu

Wafuasi 30 wa Chama cha Wananchi (CUF), leo wamefikishwa katika mahakamani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka matatu.

Wafuasi hao ni Shaban Ngurangwa (56), Shaban Tauo (29), Shaban Abdallah (40), Juma Maftar (54), Mohamed Kirungi (40), Shaweji Mohamed (39), Abdul Juma (40), Hassan Said (37), Hemed Joho (46), Mohamed Mbarouk (31), Issa Hassan (53), Allaw Ally (53), Kaisi Kais(51).

Wengine ni  Abdina Abdina (47) Allawi Msenga (53), Mohamed Mtutuma (33), Saleh Ally (43), Abdi Hatibu (34), Bakary Malija (43), Abdallah Ally (32), Said Mohamed (40), Salim Mwafisi, Salehe Rashid (29), Abdallah Said (45), Rehema Kawambwa (47), Salma Nduwa (42), Athuman Said (39), Dickson Leason (37) na Nurdin Msati (37).

Wakisomewa mashitaka yao, mbele ya Hakimu Mkazi Emilius Mchauru, wakili wa serikali Joseph Maugo akishirikiana na Hellen Mushi.

Wakili Maugo alidai katika shitaka la kwanza walilotenda wafuasi hao, inadaiwa kwamba Januari 27, mwaka huu wakiwa ndani ya Wilaya ya Temeke jijini, wafuasi hao walikula njama ya kutenda makosa ya kiuhalifu wakijua ni kinyuime cha sheria.

Akiwasomea shitaka la pili, Maugo alidai kuwa ndani ya tarehe hiyo na siku hiyo, wafuasi hao walifanya mkusanyiko usiokuwa wa halali katika Ofisi za chama chao ukiwa na lengo la kufanya maandamano bila ya kuwa na kibali.

Pia katika shitaka la tatu, Mauogo alidai kwamba ndani ya siku hiyo hiyo katika maeneo ya Mtoni Mtongani, washitakiwa wakijua ni kinyume cha sheria walifanya mgomo wa kupinga Ilani iliyotolewa  na Jeshi la Polisi ikiwataka watawanyike.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu Mchauru aliwauliza washitakiwa hao kama wanakubaliana na mashitaka waliyosomewa, lakini walikanusha kuhusika na vitendo hivyo.

Hata hivyo, wakili Maugo alidahi kwamba upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, pia hana pingamizi kuhusu kuwekewa dhamana kwa watu hao.

Upande wa utetezi ukiwakilishwa na jopo la mawakili watatu, Peter Kibatala, Hashimu Mzirai na John Malya, uliiomba mahakama kuwapa masharti nafuu washitakiwa pamoja na kusaini bondi ya kiasi kidogo.

Hata hivyo, wakili Kibatala aliiomba mahakama hiyo izingatie muda wa kuhakikiwa kwa barua za wadhamini, kutokana na idadi ya washitakiwa kuwa kubwa.

Hakimu Mchauru alikubaliana na maombi ya Kibatala na kuwataka washitakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya shilingi laki moja kwa kila mmoja.

Hakimu Mchauru aliamuru watuhumiwa hao warudishwe rumande hadi (leo), kutokana muda kuwa mdogo wa kuhakikiwa kwa barua zao za udhamini pamoja na watuhumiwa wengine kutokuwa na wadhamini.

No comments:

Post a Comment

Pages