HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 30, 2015

WAFUASI 30 WA CUF WAPATA DHAMANA




               Baadhi wa watuhumiwa wakiwa mahakamani.

Na Mwandishi Wetu


SIKU moja baada ya kusota rumande hatimaye wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wapatao 30 leo wameachiwa huru kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.

Wafuasi hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, kutenda kosa la kiuhalifu, kufanya mkusanyiko usio hlali na kugomea ilani ya polisi iliyowataka kutawanyika ambapo walirudishwa mahabusu baada ya kukosa dhamana.

Awali wafuasi hao walisota rumande juzi, baada ya kukosa dhamana kutokana na kuchelewa kuhakikiwa kwa barua za wadhamini pamoja na uwepo wa idadi kubwa ya wadhamini ambayo imesababisha muda kuwa mdogo wa kuhakiki taarifa zao.

Dhamana hiyo, ilitolewa na Hakimu Mkazi Emilius Mchauru, baada ya jopo la mwakili kutoka pande zote kati ya serikali na utetezi kuhakiki barua za wadhamini waliofika mahakamani hapo.

Hakimu Mchauru alifikia hatua hiyo, baada ya kulizishwa na kuthibitisha uahalali wa wadhamini waliojitokeza kuwawekea dhamana watu wao, ambapo masharti waliyokuwa wamepewa ni mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya shilingi laki moja kwa kila mmoja.

Baada ya kukamilika zoezi hilo, Hakimu Mchauru aliahirisha shauri hilo hadi Februari 12, mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
Waliopata dhamana ni Shaban Ngurangwa (56), Shaban Tauo (29), Shaban Abdallah (40), Juma Maftar (54), Mohamed Kirungi (40), Shaweji Mohamed (39), Abdul Juma (40), Hassan Said (37), Hemed Joho (46), Mohamed Mbarouk (31), Issa Hassan (53), Allaw Ally (53), Kaisi Kais(51).

Wengine ni  Abdina Abdina (47) Allawi Msenga (53), Mohamed Mtutuma (33), Saleh Ally (43), Abdi Hatibu (34), Bakary Malija (43), Abdallah Ally (32), Said Mohamed (40), Salim Mwafisi, Salehe Rashid (29), Abdallah Said (45), Rehema Kawambwa (47), Salma Nduwa (42), Athuman Said (39), Dickson Leason (37) na Nurdin Msati (37).

Inadaiwa kwamba kwa pamoja, wafuasi hao walitenda makosa yao Januari 27, mwaka huu katika ya Wilaya ya Temeke, ambapo walikula njama ya kutenda makosa ya kiuhalifu wakijua ni kinyume cha sheria.

Pia inadaiwa ndani ya siku hiyo, walifanya mkusanyiko usiokuwa wa halali katika Ofisi za chama chao ukiwa na lengo la kufanya maandamano bila ya kuwa na kibali.

Kosa jingine inadaiwa kwamba ndani siku hiyo wakijua ni kinyume cha sheria wakiwa maeneo ya Mtoni Mtongani, washitakiwa walifanya mgomo wa kupinga ilani iliyotolewa na Jeshi la Polisi ikiwataka watawanyike.

No comments:

Post a Comment

Pages