HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2015

MAMIA WAMZIKA MSANII MKONGWE MZEE EBBY SYKES

Baadhi ya waombolezaji wakishiriki mazishi ya msanii mkongwe, Ebby Sykes yaliyofanyika leo kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Mzee Sykes alizaliwa February 24, 1952, alikuwa mwimbaji na mpiga gitaa mashuhuri na ndiye anayemfundisha muziki mtoto wake Dully Sykes. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. (Picha na Francis Dande)
Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba (katikati) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick na kaka wa marehemu Klest Sykes wakati wa mazishi ya msanii mkongwe mzee Ebby Sykes. 
 Waziri Mkuu mstaa jaji Joseph Warioba akiweka udongo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiweka udongo katika kaburi la msanii mkongwe mzee Ebby Sykes.
 Mbunge wa Chalinzi, Riziwani Kikwete akiweka udongo.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiweka udogo katika kaburi la mzee Ebby Sykes
 Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu akiweka udongo katika kaburi la mzee Ebby Sykes.
 Dully Sykes (wa pili kushoto) akiwa ndani ya kaburi la baba yake mzee Ebby Sykes wakati wa mazishi yake.
 Ndugu na jama wakishiriki mazishi.
Umati wa watu ukiwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakati wa mazishi ya baba yake mzazi ambaye pia ni msanii mkongwe mzee Ebby Sykes.

No comments:

Post a Comment

Pages