HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2015

WAKUU WA WILAYA WAPYA KUPIMWA UTENDAJI WAO MIEZI SITA


Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imewapa muda wa miezi sita Wakuu wapya wa Wilaya waliyoteuliwa hivi karibuni ili kupima utendaji wao wa kazi.

Mapema wiki hii Serikali iliteuwa Wakuu wa Wilaya na wengine wazamani kuhamishwa vituo vipya vya kazi.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake mkoa wa Iringa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakuu hao wapya amesema watapimwa kwa miezi sita hadi pale watakapomaliza ujenzi wa vyumba vya Maabara ya shule zilizopo vituo vyao vya kazi.

"Tulimshauri uteuzi huu ufanyike baadaye kutokana Madc wengine wanaendelea na ujenzi wa Maabara, lakini Rais akasema hawa wapya watamalizia viporo vilivyoachwa kwa  kipindi cha miezi sita, tutawapima kwa muda huo" alisema Waziri Pinda.

Kwa mujibu wa Waziri muda huo unatosha kwa Madc wapya kupimwa kiutendaji wa kazi yao.

No comments:

Post a Comment

Pages