HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2015

ALBINO WAVURUGA MKUTANO WAO NA RAIS KIWETE

Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Nchini, Ernest Kimaya (wa pili kulia) akiondolewa baada yakumpiga teke mmoja wa albino, Nuru Chagutu katika Barabara ya Magogoni jirani na Ikulu Dar es Salaam. Baadhi ya watu wakiamulia ugomvi uliotokea kati ya wanachama na viongozi wao.
Ofisa wa Ikulu akiwazuia Albino baada ya kutokea mtafaruku na viongozo wao kabla ya kuingia Ikulu ambapo Rais Kikwete alikuwa na mazungumzo na baadhi ya viongozi wao.
Watu wenye ulemavu wa ngozi wakijaribu kutupiana makonde nje ya Ikulu muda mfupi kabla ya kwenda kuonana na Rais Jakaya kikwete ambaye alikuwa na mazungumzo nao.

Na Mwandishi Wetu

WATU wenye ulemavu wa ngozi Albino, leo walizusha vurugu katika viwanja vya Ikulu wakipinga baadhi ya wao kuonana na Rais Jakaya Kikwete.

aliyekuwa akizuiwa asipigane ni Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Nchini, Ernest Kimaya
baada kumpiga teke mmoja wa albino, Nuru Chagutu katika Barabara ya Magogoni Dar es Salaam.

Kundi la albino waliokuwa wamebaki nje walianza kupaza sauti na kudai waliopewa nafasi ya kuingia kuonana na Mh. Rais si viongozi wao, jambo ambalo liliwalazimu maofisa Usalama kuingilia kati.

Katika mkutano huo Rais Kikwete alikutana na wawakilishi 15 huku wengine zaidi ya 30 wakiwa na kuanza kupaza sauti zao na kusema kuwa walioingia ndani sio viongozi wao kwani muda wao ulishakwisha hivyo ni bora wakatoka kabla hawajaanzisha vurugu kubwa katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages