HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 25, 2015

TGNP YATAKIWA KUBADILISHA MFUMO WA UFUNDISHAJI

NA KENNETH NGELESI, MBEYA

WITO umetolewa kwa TGNP Mtandao kubadilisha mfumo wa ufundishaji  kwa kutumia picha zinazoonesha ukatili na unyanyasaji kwa wanawake hali ambayo inawafanya kuendelea kuwa wanyonge.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki katika kikao  cha mrejesho  wa utafiti raghibishi na vituo vya taarifa na maarifa  kilichowahusisha    watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,baadhi ya wananchi wa Kata ya Nsalala katika Mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi,mkoani Mbeya.

Ofisa  Masoko Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,Daud Mwalusamba alisema kuwa  matumizi ya picha zinazowaathiri wanawake kisaikolojia  katika utoaji wa elimu  mbalimbali kwani zinachangia kwa asilimia kubwa wanawake kuendelea kujiona  wanyonge zaidi.

Mwalusamba ametoa ushauri  huo kutokana na utafiti mdogo  alioufanya kwa baadhi ya vikundi vya wanawake  na kwamba upo  umuhimu wa kuonesha picha zenye mfano wa kuigwa  kama za  wanawake maarufu waliopata mafanikio duniani.

Kwa upande wake Mwakilishi wa kutoka TGNP Mtandao,Rehema Mwateba  ametoa ufafanuzi  kuhusiana  na suala hilo alisema inategemea mapokeo na kutafsri.

Hata hivyo  Ofisa uhusiano  wa TGNP Mtandao,Merczedeck Karol  alisema mikakati ya mtandao huo ni kwamba suala hilo aliona na watalifanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

Pages