HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 25, 2015

TPAWU wampasha Waziri; Wadai Mwekezaji Mtibwa amefilisika

Na Bryceson Mathias, Mvomero, Morogoro


CHAMA cha Wafanyakazi mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU), wamempasha Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makala, wakidai, aiambie Serikali kuwa Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa, amefilisika, hawezi kuendesha Kiwanda, na Serikali ipeleke Mwekezaji mwingine.


Akizungumza katika Mkutano wa Wafanyakazi, akiwepo Meneja wa Kiwanda cha Mtibwa, Hamad Yahaya, Kiongozi wa TPAWU Kanda na Waziri huyo, Mwenyekiti wa Tawi la TPAWU Mtibwa, Dominick Mbasha, alisema Mwekezaji huyo ameshindwa, Serikali ipeleke Mwekezaji mwingine.


Katika Mkutano huo ambao, Waziri Makala alitakiwa aongozane na Mawaziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Masatu Wasira, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda, alishindwa kumaliza Mgomo huo, na Wafanyakazi kuapa kuendelea kupiga Kambi langoni kwa mwekezaji hadi walipwe.


Mbali ya Makala kusema Mwekezaji anapaswa kuwalipa wafanyakazi hao, alisema amemuomba ruhusa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aende kutatua Mgomo huo, na akirejea ampe taarifa, huku akidai Mawaziri, Wassira na Dkt. Kigoda, wameshindwa kufika kwa sababu ya kazi Maalum.


Pamoja na Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Yahaya, kumuahidi Waziri Makala kuwa ataanza kuwalipa Mishahara wafanyakazi hao siku inayofuata hivyo warejee kazini, Wafanyakazi waligoma kuondoka wakidai, Meneja huyo si Mkweli, hivyo watakesha  hapohapo hadi watakapolipwa.


Kwa Mara nyingine, Makala alitaka kutumia Sarakasi alizotumia awali za kuita utitiri wa Mawaziri husika na kero
zinazomsumbua katika jimbo lake kama alivyofanya kwenye Mauaji ya Wakulima na Wafugaji wa Bonde la Mpunga Mgongola, ili kuwatumainisha wananchi, lakini safari hii alikwama.


Awali aliwakokota, aliyekuwa Waziri wa mifugo Dkt. David Mathayo, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani Dkt. Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Ushirika, Mhandisi, Christopher Chiza, na yeye Makala ili kutatua Mgogoro wa Wafugaji na Wakulima, lakini hadi leo utatuzi huo bado ni ndoto za Mchana

Maisha ya Wafanyakazi na Wakulima wadogo wa Miwa wa Mtibwa, yamekuwa ya ukatili na unyanyaswaji Mkubwa na kupindukia wanaofanyiwa na Mwekezaji huyo, kiasi kwamba wanaweza kufanya kazi akawalipa anavyotaka bila kujali utu na shida walizonazo.

No comments:

Post a Comment

Pages