HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 02, 2015

Ulrich Urio:Tamasha la Pasaka liwakumbuke wanyamapori

Na Mwandishi Wetu

MENEJA wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Ulrich Urio ametoa wito kwa waandaaji wa Tamasha la Pasaka kuelekeza nguvu zao kupigia kelele wanyama wenye uhitaji maalum wanaomalizwa kila kukicha katika mbuga zetu za hifadhi.

Kwa mujibu wa Urio wanyamapori hivi sasa katika wakisikia milio ya gari  na bunduki huanza kukimbia hovyo kusaka hifadhi, jambo ambalo linachangia kupoteza maliasili za Tanzania kama Tembo, Faru na wanyama wengineo.

Urio alisema sambamba na Msama pia wito wa kuwalinda wanyama wetu unatakiwa kuongezewa nguvu pia na Chama cha Kutetea haki za Wanyama kwa sababu hivi sasa idadi kubwa ya wanyama wanauawa na majangili ambao wana nia ovu na Tanzania.

Alisema wanyama wenye uhitaji kama Tembo sasa hivi hata kuonekana kwake ni kwa nadra kwa sababu ya kuwindwa lakini wanyama kama Simba huranda porini kwa sababu mahitaji yao hayafanani na Tembo.

Kuhusu mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi ‘albino’ alitoa wito kwa vyama na taasisi zinazoguswa na mauaji ya walengwa hao vitoe tiba ama ufuatiliaji wao usiishie kupiga kelele zisizo na mwelekeo na badala yake ziongeze ufanisi kwa kuwalinda ipasavyo wahusika hao.

Urio alimalizia kwa kumpongeza Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kwa kuwa karibu zaidi na jamii ambayo ina uhitaji maalum na kumuomba aongeze ufanisi zaidi katika kutekeleza majukumu yake.

No comments:

Post a Comment

Pages