HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 10, 2015

MGOMO WA MADEREVA WATINGISHA NCHI LEO

Moto uliowashwa katikati ya barabara katika eneo la Stendi ya mkoa Ubungo jijini Dar es Salaam kufuatia mgomo wa madereva wa mabasi yaendayo  mikoani pamoja na daladala. (Picha na Francis Dande) 
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa wameimarisha ulinzi wakati wa mkutano wa viongozi wa serikali na madereva waliokuwa katika mgomo wa kuishinikiza serikali kusikiliza madai yao. (Picha na Loveness Bernard)
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka akizungumza na madereva waliokuwa katika mgomo wa madereva wa mabasi ya mikoani, malori, mabasi yaendayo nchi jirani na daladala ili kuishinikiza serikali kusikiliza madai yao. (Picha na Francis Dande)
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani akijiandaa kupiga bomu la machozi ili kuwatuliza wananchi waliokaidi amri ya Jeshi la Polisi ya kuwataka kutawanyika Stendi ya Mkoa Ubungo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Kamishina wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova akiwasili katika eneo la Stendi ya mkoa Ubungo jijini Dar es salaam jana wakati wa mgomo wa madereva wa mabasi, malori pamoja na daladala. (Picha na Loveness Bernard)
Mmoja wa waathirika wa vurugu zilizotokea wakati wa mgomo wa madereva akipata huduma ya kwanza baada ya kupoteza fahamu kutokana na mlipuko wa mabomu ya machozi. (Picha na Francis Dande)
Umati wa watu ukimsikiliza Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (hayupo pichani) wakati akizungumza na madereva ili kufikia muafaka kutokana na mgomo huo. (Picha na Francis Dande)
Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa Malori, Shaban Mdemu akiwa amebebwa  na madereva mbalimbali waliokuwa katika mgomo huo. (Picha na Loveness Bernard)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akizungumza na madereva waliokuwa katika mgomo. Kushoto ni Kamishina wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova. (Picha na Loveness Bernard) 
 Mabasi yakianza safari baada ya madereva waliokuwa katika mgomo kusitisha mgomo huo.
 Wananchi wakishuhudia mabasi yakianza safari.
 Mabasi yaliyokuwa katika mgomo yakiwa yameegeshwa katika Stendi ya Mkoa kaba la kufikia muafaka na serikali.
 Mabasi yakiendelea na safari za kwenda mikoani na nchi jirani baada ya mgomo kumalizki.

No comments:

Post a Comment

Pages