HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

April 28, 2015

THAMANI YAPOROMOKA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 20

 Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za bunge jijini Dar es Salaam kuhusu kuporomoka kwa thamani ya shilingi.

James Mbatia akifafanua jambo.

Na Mwandishi Wetu

 Thamani ya shilingi ya Tanzania imekuwa ikiporomoka kwa kasi ya kutisha ambapo ndani ya mwezi mmoja imeporomoka kwa zaidi ya asilimia 20 kutoka shilingi 1650 kwa Dola moja ya Kimarekani hadi shilingi 2010 kwa takwimu za jana.

Kuporomoko huko ni tishio kwa uchumi wa nchi. Sayansi ya anuai inatuonyesha kwamba nguvu ya mporomoka wa kiasi hiki, inaweza kutikisa vibaya mfuno wa wa uchumi kama hatua za kifedha hazitachukuliwa haraka iwezekanavyo na taasisi husika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri Fedha Kivuli, James Mbatia amesema kuwa "Yapo mambo mengi yanayoweza kusababisha poromoko la aina hii, mambo ya ndani na mambo ya nje ya nchi." aliongeza kuwa 'poromoko tunalozungumzia sasa linasababishwa zaidi na mambo ya ndani, hivyo basi mpira uko mikononi mwetu na wachezaji ni sisi na uwezo wa kukabili poromoko la shilingi yetu tunao.'    

No comments:

Post a Comment

Pages