HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 24, 2015

NSSF YAENDESHA KAMBI YA KUPIMA AFYA BURE MKOANI TANGA

Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), litaendesha  kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Tanga.

Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Zoezi hili litakaloanzia mkoani Tanga. 

Linatarajiwa kwenda Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.Zoezi litaanza viwanja vya Tangamano kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.  

HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma mbalimbali zitatolewa bure kwenye kambi hizi zikiwemo;
  1.      Upimaji wa Shinikizo la damu
  2.      Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
  3.      Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Uzito)
  4. ·    Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo
  5. ·    Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
  6. ·     Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.

 Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.
NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa Tanga kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Wavuvi,  Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.
Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.
Wananchi wa Tanga wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.

NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
 Meneja wa Mafao ya Matibabu (SHIB) Dk.Ali Mtulia akizungumza na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali juu ya lengo la kambi ya upimaji Afya kwa wakazi wa Tanga ambayo inaendelea Mkoani Tanga kwenye Viwanja vya Tangamano.
Daktari Mtulia (kulia ) na Dk.Limu (kushoto) wakipima uzito na Urefu wa Mkazi wa Tanga ili kuweza kujua na kumshauri juu ya uwiano wa Urefu na Uzito wake.
 Daktari bingwa wa Siku nyingi Dk. Ali Mzige akimshauri mkazi wa Tanga juu ya afya yake na lishe bora.
 Afisa Matekelezo mkoa wa Tanga, akimuandikisha mmoja wa wakazi wa Mkoa wa Tanga aliyepimwa Afya na kuamua kujiandikisha kwa hiari na Mfuko wa NSSF ili aweze jipatia matibabu bure.
 Wakazi wa Tanga wakipewa Elimu ya pamoja kabla hawajaamua kupima kwa Hiari Virusi vya Ukimwi katika zoezi la upimaji afya bure linaloendeshwa na NSSF.
Wakazi wa Mkoa wa Tanga waliokuja kupima Afya zao kwa Hiari wakisubiri kuwaona madaktari wa NSSF katika viwanja vya Tangamano.

No comments:

Post a Comment

Pages